LIGI YA MABINGWA ULAYA : ARSENAL USO KWA USO NA BAYERN MUNICH, MAN CITY YAPANGWA KUNDI LA KIFO.





Kwa mara ya tatu katika misimu minne ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya Arsenal watakutana tena na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika mechi za kundi F zilizopangwa jana nchini Ufaransa.

Manchester United wamepangwa kukutana na timu ya zamani ya mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Memphis Depay klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi.

Mabingwa wa England Chelsea wamepangwa kukutana na FC Porto ya Ureno klabu ambayo ilishawahi kuchukua ubingwa wa Ulaya mwaka 2004 wakiwa na Jose Mourinho kama kocha.

Manchester City wao wamepangwa katika kundi la kifo wakikutana na Juventus ambao ni mabingwa wa Italia, Sevilla ambao ni mabingwa wa Europa na Borussia Monchengladbach ya Ujerumani.

Mabingwa watetezi Barcelona wao wamepangwa katika kundi E wakiwa pamoja na Bayer Leverkusen, AS Roma na Bate.

Kila timu katika makundi hayo itacheza mechi sita katika hatua hii ya makundi ambayo itaanza kuchezwa tarehe 15 na 16 mwezi Septemba.

MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Group A: 
Paris St-Germain, Real Madrid, Shakhtar Donetsk, Malmo

Group B: 
PSV Eindhoven, Manchester United, CSKA Moscow, VfL Wolfsburg

Group C:
 Benfica, Atletico Madrid, Galatasaray, Astana

Group D:
 Juventus, Manchester City, Sevilla, Borussia Monchengladbach

Group E: 
Barcelona, Bayer Leverkusen, AS Roma, BATE Borisov

Group F: 
Bayern Munich, Arsenal, Olympiakos, Dinamo Zagreb

Group G: 
Chelsea, Porto, Dynamo Kiev, Maccabi Tel-Aviv

Group H: 
Zenit St Petersburg, Valencia, Olympique Lyon, Gent

No comments

Powered by Blogger.