LICHA YA KUPIGWA BENCHI MAN UNITED, DE GEA AITWA KIKOSINI SPAIN


Licha ya kupigwa benchi na klabu yake ya Manchester United kipa David De Gea ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Spain kinachojiandaa na mechi mbili za kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Ulaya 2016 kundi C dhidi ya Slovakia na Macedonia.

De Gea ameachwa katika mechi 5 ambazo United imecheza msimu huu huku Sergio Romero akipewa nafasi baada ya sakata lake la kutaka kuihama klabu hiyo kutofikia mwafaka mpaka sasa.

Akizungumzia uamuzi wa kumwita kipa huyo kocha Vicente Del bosque anasema "Naamini kinachomkuta De Gea hivi sasa ni hali ya mpito tu na natumai siku si nyingi atarejea" 

KIKOSI KAMILI CHA SPAIN


Magolikipa: 
Casillas (Porto), De Gea (Manchester United), Rico (Sevilla)

Mabeki:
Alba (Barcelona), Azpilicueta (Chelsea), Bartra (Barcelona), Bernat (Bayern), Carvajal (Real Madrid), Juanfran (Atletico Madrid), Pique (Barcelona), Ramos (Real Madrid); 

Viungo:
Busquets (Barcelona), Cazorla (Arsenal), Fàbregas (Chelsea), Iniesta (Barcelona), Isco (Real Madrid), Koke (Atletico Madrid), Mata (Manchester United), Silva (Manchester City), Vitolo (Sevilla); 

Washambuliaji:
Costa (Chelsea), Pedro (Chelsea), Alcacer (Valencia).

No comments

Powered by Blogger.