KIJIWE CHA WAPENDA SOKA : TATHMINI ARSENAL VS LIVERPOOL


Kuelekea pambano la ligi kuu nchini England baina ya Arsenal na Liverpool hii ndiyo tathmini ya Wapenda Soka katika mtandao wa Whatsapp

AMEANDIKA FAUROJO

 Liverpool the main man benteke ataamua matokeo ya liverpool akipata chance anakuua. Nataka nimuone mhuni Firmino leo

Naipa ushindi Arsenal wa goli 3-1 wana kikosi kizuri na attacking force nzuri ikiongozwa na Sanchez kiungo mchezeshaji kama mesut ozil akina cazorla Ramsey wapo deadly safu ya ulinzi nyuma koss na Per beki zao za kulia na kushoto mchezaji kma ballerin mwenye pace pia ya kupeleka mashumbulizi mbele

AMEANDIKA SAYEED GAGU

Mi nategemea match yenye kasi sana aisee liverpool hii sio ile wamejaribu kusuka kikosi chao vzr katika safu ya ushambuliaji . Na kumekuwa na watu wengi kuanzia kwa kiungo mchezeshaji na steikers kuliko huku nyuma.. match mbili za nyuma liver wamezuia vzr lakini bado nina mashaka sana na safu yao ya ulinzi hii ni kutokana na kukosa natural holding midfielder

Utabiri wangu mimi naona arsenal akiondoka na ushindi wa goli 2 kwa moja

AMEANDIKA MUHSIN HERO


Ni mechi nzuri sana kuitazama leo hasa ukizingatia historia ya timu hzi.

Arsenal amekuwa na historiamnzuri kwa miaka ya hv karibuni hasa dhid ya liverpool na Emirates panawapa kichwa arsenal na kwao imekuwa ni nguzo katika ushindi. Lakini umahiri wa viungo na kasi ya sancezi ndyo vitatoa matokeo leo.

Upande wa liverpool mchezo wao wa kasi na pasi za haraka unaweza kuwa hatari kwa arsenal. Ila ushindi wao leo unategemea zaid akili ya countho na umahiri wa benteke.

Karata yangu naitupa kwa arsenal

Arsenal 2-1 liverpool

AMEANDIKA EDO DC

Mtihani wa kwanza kwa Liverpool katika harakati zao za kurudi tena katika Ligi ya Mabingwa barani ulaya kwa kuingia katika TOP. Kama Liverpool wanataka kuipima timu yao kiubora basi wanapaswa kushinda mechi hii

Wanakutana na wataalamu wa Top 4 Arsenal katika dimba ambalo mechi ya ufunguzi iliwaliza Arsenal hapo baada ya kuzibuliwa bao 2-0 na West Ham.

Uwanja wa Emirates umekua mgumu sana kwa Liverpool kwani katika mechi 15 walizotembelea Emirates walitembezewa kichapo mara 8 mara 6 wakiambulia sare na ushindi kwao ni mara 1 tu.

Kocha Brendan Rodgers hajawahi kushinda katika mechi zote 4 alizotembelea Katika uwanja wa Emirates akifungwa mara 3 na kutoka sare mara 1.

Mechi baina ya timu hizi huzalisha magoli mengi historia inasema hivyo kwani kumekua na "hat trick" 5 hakuna timu zilizowahi kufikia rekodi hiyo katika historia ya ligi kuu nchini England.

Mara ya mwisho Arsenal kupoteza mechi mbili mfululizo wakiwa katika uwanja wa nyumbani ilikua msimu wa mwaka 1949/1950 ambapo Tanzania ilikua haijapata hata Uhuru sasa swala la kufungwa leo silioni kwa Arsenal.

Kama Giroud akicheza leo itakua mechi yake ya 99 katika ligi tangu atue Arsenal akitokea Montepellier ya Ufaransa na kwa taarifa yako tu jamaa ameshatupia magoli 42 katika mechi hizo 99 na katika Historia ya Arsenal anazidiwa na Thierry Henry mwenye magoli 59 Ian Wright (56) na Emmanuel Adebayor (44) ambao waliyafunga magoli hayo katika mechi zao 100 za kwanza wakiwa na Arsenal.

Kipa wa Liverpool Simon Mignolet ndiye kipa bora kabisa kwa mwaka 2015 akiwa hajaruhusu kufungwa goli lolote katika michezo 11 hakuna kipa aliyeifikia rekodi hii kuanzia Januari mpaka sasa katika ligi kuu nchini England.

Mimi Edo natabiri kuwa mchezo wa leo utamalizika kwa
ARSENAL 3-2 LIVERPOOL

AMEANDIKA ZAHIR BILAL

Liverpool bado hawana muunganiko mzuri wa kucheza kitimu wamepata matokeo katika mechi mbili zilizopita lakini bado hawatengenezi nafasi nyingi za kufunga..

 bado hawapo vizuri katika eneo la mwisho la adui na beki pia hasa upande wa kushoto ule nadhani leo Moreno ataanza baada ya yule Gomez..Lovren siku yake leo ya kuwanyamazisha wakosoaji wake alikua na msimu mbaya mwaka uliopita bado hajaitendea haki ile £20m

Wenger anaweza kuanza na Ox au Walcott kujaribu kutumia udhaifu wa Liverpool ule upande wa kushoto

kiungo cha arsenal ni timilifu kuliko kile cha Liverpool natarajia kitawapa shida sana..Coutinho,Carzola,Ozil hawa wanaweza kuiamua hii mechi iende upande upi..Milner na Hendo pia hawatakiwi kuwa chini ya kiwango chao kama Liverpool watataka kupata matokeo leo..

nafikiri pia Rodgers umefika muda wa kumchezesha Can kwenye kiungo pamoja na Hendo yule Milner acheze  pembeni sasa zile krosi zake miguu na kichwa cha Benteke vinazihitaji zaidi na hata Firmino weka kushoto kule umtie Belerrin wasiwasi wa kwenda mbele kila wakati,nyuma ya Benteke weka Coutinho ili timu iwe na dynamism  Brendan aachane na 3  5 2

1-1 mwisho wa siku

makocha wote sio watu wa kukabia chini ya duara kubwa natarajia mechi yenye mashambulizi makali pande zote mbili

AMEANDIKA MARTIN KIYUMBI

Baada ya Steven 8 kuondoka, nahc mpenzi wake Countinho alimwambia Countinho anataka akiwa na shoga zake awe anajidai kuwa mpenzi wake ni Mfalme wa Anfield. Ndo kitu ambacho Countinho anajitahidi kumpatia Mpenzi wake.

Arsenal inakutana na liverpool yenye Countinho ambaye kiwango chake kimeongezeka mara mbili kulinganisha na mechi ya mwisho waliyokutana.  Mechi hii binafsi macho yako yanawasha kuona mpira ukiwa mguuni mwa Countinho na Ozil kuliko goli la Giroud.

Countinho na Ozil ndio watakaoamua mchezo wa leo. Matokeo ya mechi ya leo yatatokana na hawa jamaa walivyoamka asubuhi ya leo.

Mchezo wa mwisho wa msimu jana ambao Arsenal ilishinda goli 4, ilikutana na liverpool iliyokuwa haina kiongozi mzuri na beki wa kati mzuri. Lakini liverpool ya mechi mbili zilizopita ina Martin ambaye aliye katika kiwango bora.

 Na suprise kubwa kwa liverpool msimu huu ni kiwango bora cha Lovren. Kwa hiyo ukilinganisha beki ya Toure na Can ya msimu uliopita mechi ya mwisho na beki hii ya mechi mbili zilizopita ya Martin na Lovren utagundua kabsaa ugumu wa Arsenal kupata matokeo ni mkubwa. Upacha wa Martin na Lovren umefana kabsaa . Kwangu mimi ukiniuliza nikutajie Beki pacha za kati nilizofurahia kuziona msimu huu lazima nikutajie hii ya lovren na Martin baada ya Mangala na Kompany, Smaling na Blind.

ASANTENI NA TUKUTANE SIKU NYINGINE

No comments

Powered by Blogger.