ARSENAL NA LIVERPOOL HAKUNA MBABE.


Mabingwa wa kombe la FA Arsenal imelazimishwa sare ya bila kufungana na Liverpool katika pambano kali la ligi kuu nchini England lililopigwa katika dimba la Emirates nyumbani kwa Arsenal.

Pambano hilo lililoshuhudia ufundi wa magolikipa katika kuokoa michomo ya wazi kabisa Petr Cec akiwa shujaa wa Arsenal kipindi cha kwanza wakati Simon Mignolet yeye shughuli yake ilionekana zaidi kipindi cha pili.

Kila timu ilicheza kwa tahadhari kubwa kuepuka kufungwa bao lolote huku washambuliaji wa Liverpool wakiongozwa na Benteke na Coutinho huku Arsenal wakiongozwa na Giroud na Alexia Sanchez.

Kwa matokeo hayo Liverpool wamepanda mpaka nafasi ya tatu huku Arsenal ikiwa ya 9 katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini England.

++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.