GOLI LA KUJIFUNGA LA NEWCASTLE LAWAPA ARSENAL POINTI 3 MUHIMU
Goli la kujifunga la nahodha wa Newcastle United Fabricio Coloccini limeipa Arsenal pointi 3 muhimu katika ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi mchanacwa leo dhidi ya Newcastle.
Mchezo huo wa ligi kuu ya England katika uwanja wa St. James Park umeifanya Arsenal kufikisha pointi 7 muhimu baada ya kucheza michezo minne.
Arsenal ilipata bao hilo pekee kipindi cha pili baada ya shuti la Alex Oxlade-Chamberlain kumgonga beki na nahodha huyo wa Newcastle Coloccini na kutinga wavuni.
Licha ya Newcastle kubaki kumi uwanjani baada ya Aleksandar Mitrovic kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 16 baada ya kumchezea faulo kiungo wa Arsenal Francis Coquelin.
Ushindi wa Arsenal dhidi ya Newcastle ambao hawakufaniwa kupiga shuti lolote golini kwa Arsenal umeifanya klabu hiyo ya London kuendeleza wimbi la ushindi katika uwanja wa St James' Park tangu mwezi Decemba 2005 wakishinda mechi zote 8 na kufunga magoli 21na kufungwa magolin6 tu.
No comments