CHELSEA NA LIVERPOOL ZAAMBULIA VICHAPO PAMOJA NA MATOKEO NA WAFUNGAJI WA MECHI ZOTE ZA LEO ENGLAND
Mzunguko wa nne wa ligi kuu nchini England ulianza leo kwa mechi 8 kupigwa ambapo magoli 16 yamefungwa huku kukishuhudia vigogo vya ligi hiyo vikiendelea kuanguka.
Chelsea wakiwa nyumbani wamekubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Crystal Palace huku Liverpool ambao msimu huu wamesajili wachezaji wengi wakiambulia kichapo pia cha bao 3-0 toka kwa Wagonga nyundo wa London klabu ya West Ham.
Baada ya mechi za leo Msimamo kamili wa ligi hiyo unaonyesha kuwa Manchester City wanaongoza wakiwa na pointi 12 baada ya michezo minne wakifatiwa na Crystal Palace wenye pointi 9 huku Leicester City wakiwa katika nafasi ya tatu na pointi zao 8.
Arsenal iliyoibuka na ushindi leo imepanda mpaka nafasi ya 5 wakiwa na pointi 7 baada ya kucheza michezo minne Wakati Chelsea wao wako katika nafasi ya 13 wakiwa na pointi 4
MATOKEO NA WAFUNGAJI MECHI ZOTE LEO.
Newcastle United 0-1 Arsenal
- Fabricio Coloccini (52') OG
AFC Bournemouth 1-1 Leicester City
- Callum Wilson (24')
- Jamie Vardy (86') P
Aston Villa 2-2 Sunderland
- Yann M'villa (8')
- Scott Sinclair (11')P (41')
- Jeremain Lens (52')
Chelsea 1-2 Crystal Palace
- Bakary Sako (65')
- Radamel Falcao (79')
- Joel Ward (81')
Liverpool 0-3 West Ham United
- Manuel Lanzini (3')
- Mark Noble (29')
- Diafra Sakho (90')
Manchester City 2-0 Watford
- Raheem Sterling (47')
- Fernandinho (56')
Stoke City 0-1 West Bromwich Albion
- Jose Salomon Rondon (45')
Tottenham Hotspurs 0-0 Everton
No comments