CAPITAL ONE CUP : ARSENAL USO KWA USO NA TOTTENHAM


Mabingwa wa kombe la FA nchini England klabu ya Arsenal imepangwa kucheza mechi yake ya mzunguko wa tatu wa kombe la Ligi maarufu kama Capital One dhidi ya wapinzani wao wa jadi Tottenham Hotspurs.

Timu zote hizo zinatoka katika jiji la London na zimekua na upinzani mkali zinapokutana na safari hii watakutana katika mechi ya mapema katika michuano hiyo ikichezwa katika dimba la White Hart Lane na mshindi atapita kwenda katika hatua ya nne na zikitoka sare basi watacheza mechi ya marudiano katika uwanja wa Emirates.

Mabingwa watetezi wa kombe hilo Chelsea wao wamepangwa kucheza na klabu ya daraja la pili ya Walsall mechi ikichezwa katika dimba la klabu hiyo.

Manchester United watakua nyumbani Old Trafford kuikaribisha Swindon Town, Man City wao watakua ugenini kucheza na Sunderland wakati Liverpool wataikaribisha Carlisle

Ratiba kamili ya mechi hizo iko hivi...👇🏿👇🏿👇🏿

Man United v Ipswich Town
Liverpool v Carlisle
Crystal Palace v Charlton
Middlesbrough v Wolves
Norwich v West Brom
Hull v Swansea
Leicester v West Ham
Aston Villa v Birmingham
Tottenham v Arsenal
Sunderland v Man City
Newcastle v Sheffield Wednesday
Reading v Barnsley/Everton
Preston v Bournemouth
Walsall v Chelsea
MK Dons v Southampton
Fulham v Stoke City


👉🏿Mechi za Raundi hii ya 3 zitachezwa Wiki ya
kuanzia Septemba 21.


No comments

Powered by Blogger.