MAN UNITED YAJIANDAA KUMPOTEZA DE GEA YAMNASA KIPA ALIYEWAPELEKA ARGENTINA FAINALI KOMBE LA DUNIA


Katika kile kinachoonekana ni kujiandaa kumpoteza kipa wake namba moja David De Gea klabu ya Manchester United imemsajili bure kabisa kipa aliyeipeleka Argentina katika fainali za kombe la Dunia mwaka jana Sergio Romero.

Romero amesaini mkataba wa miaka mitatu kukipiga ndani ya Old Trafford kukiwa pia na makubaliano ya mwaka mmoja wa nne iwapo atafanya vizuri amejiunga na United akitokea klabu ya Sampdoria ya Italia baada ya mkataba wake kumalizika.

Wakati huu ambapo David De Gea anaweza kutimkia Real Madrid Romero anatarajiwa kuwa mbadala wake au kama De Gea atabaki basi atakua kipa namba mbili kwani Victor Valdes anaweza kuondoka klabuni hapo baada ya kutibuana na kocha Luois Van Gaal aliyemtaka akafanye mazoezi na kikosi cha wachezaji wenye umri wa miaka chini ya 21.
Romero alishawahi kusajiliwa na kocha Louis Van Gaal mwaka 2007 wakati huo van Gaal akiifundisha AZ Alkmaar ya Uholanzi akitokea Racing Club ya Spain

No comments

Powered by Blogger.