KOCHA KERR AANZA KAZI RASMI LEO
Kocha mpya mzungu Raia wa uingereza Dylan Kerr ameanza rasmi leo kazi ya kukinoa kikosi hicho katika viwanja vya sigara kazi. Kocha huyo alifika leo kwa lengo la kuwafahamu wachezaji wake pamoja na kukutana na benchi lake ambalo ataliongoza katika msimu wa 2015-2016.
Simba imedhamiria kurudisha makali yake na hadhi yake kwa kuunda upya benchi lake la ufundi pamoja na kusajili wachezaji wazuri kwa ajili ya kuisaidia simba.
Kazi kubwa kwa mwingereza uyo ni kuirudisha Simba katika Ramani ya soka na medani ya kimataifa.
No comments