KABLA HUJALALA KAMATA HABARI HIZI ZA USAJILI SIKU YA LEO BARANI ULAYA



Matajiri wa Jiji la Paris klabu ya PSG wanajipanga kumtumia beki wa kulia wa timu hiyo Gregory Van Der Wiel kwenda Man United katika harakati za kumsajili Angel Di Maria.

Christian Benteke anapanga kumwambia kocha wake Tim Sherwood kama anataka kuihama Aston Villa wakati atakaporudi mazoezini kesho Jumatano. Yasemekana Liverpool wako katika nafasi nzuri ya kumshawishi Kijana huyo wa Ubelgiji kujiunga nao.

Dili la paundi milioni 20 ambalo Chelsea walikua wameliandaa kumnasa kiungo wa Spain na klabu ya Real Madrid Isco limekataliwa na Real Madrid. Kocha wa Chelsea Jose Mourinho yuko tayari kumpeleka Oscar na pesa ili kupata saini ya kiungo huyo.

Usajili unaendelea kwa upande wa Liverpool na hivi leo zimetoka taarifa kwamba kocha Brendan Rodgers ametenga paundi milioni 16 kumpata mshambuliaji wa Man City Stevan Jovetic ambaye dau lake linaonekana ni rahisi kuliko dau la Benteke ambaye anawaniwa pia na Liverpool.

Wakati huo huo mshambuliaji wa timu hiyo (Liverpool) Mario Balotelli ameshindwa kujiunga  na wenzake wanaojiandaa na msimu mpya baada ya kupewa ruhusa ya kushughulikia maswala ya kifamilia.

Winga wa Schalke 04 ya Ujerumani Sidney Sam ameferi vipimo vya afya na kushindwa kujiunga na Eintracht Frankfurt .

Celtic ya Scotland iko katika nafasi nzuri kumsajili kinda wa Real Madrid Martin Odegaard kwa mkopo wa msimu mzima. Mchezaji huyo alisajiliwa mwaka jana toka katika klabu ya Norway Stromsgodset.

Juventus wamekamikisha usajili wa Simonne Zaza kwa ada ya uhamisho paundi milion 12.75 na mkataba wa miaka mitano akitokea klabu ya Sassuolo.

USIKU MWEMA

No comments

Powered by Blogger.