HABARI MPYA ZA USAJILI BARANI ULAYA ASUBUHI HII
Mshambuliaji wa Manchester United Robin Van Perse amekubali kusaini mkataba wa miaka minne na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki dili hili likitarajiwa kutangazwa kabla ya wikiend hii. Van Perse ataungana na Luis Nani ambaye ameshatimkia katika klabu hiyo. Mkataba wa mchezaji huyo katika klabu ya Man United ulikua unafikia ukingoni na kwa umri wake ilikua ngumu kupewa mkataba wa muda mrefu
Uwezekano wa mshambuliaji Shaun Wright Philips kujiunga na New York Red Bulls ya Marekani umeingia do baada ya kocha wa Timu hiyo Jesse Marsch kupuuzia habari za kumwania nyota huyo aliyeachwa na QPR ambaye alitaka kuungana na kaka Yake Bradley anayeichezea timu hiyo.
Mshambuliaji kinda wa Man United Michael Keane amepelekwa kucheza kwa mkopo katika klabu ya Championship ya Preston. Keane ameichezea Man United mara moja tu mwaka 2011 na muda wote huo amekua akipelekwa kucheza kwa mkopo.
Kuna uwezekano mkubwa kwa mshambuliaji Gonzalo Higuain akajiunga na mabingwa wa kombe la FA Arsenal baada ya taarifa nyingi kumuhusisha leo na klabu hiyo.
Newcastle wako katika mazungumzo na PSV Eindhoven kuhusu usajili wa nahodha Georginio Wijnaldum japokua hakuna kiasi cha pesa kilichowekwa wazi kukamilisha dili hilo.
Danny Ings amefunguka leo akisema kuwa atakua mwenye furaha sana kucheza na mshambuliaji Daniel Sturridge katika klabu ya Liverpool.
Nahodha wa Arsenal Mikel Arteta amesaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi kuichezea Arsenal na kocha wa timu hiyo Arsenal Wenger amethibitisha kuwa Arteta ataendelea kuitumikia Arsenal.
Usajili wa kipa wa Real Madrid Ike Casillas kwenda FC Porto unaelekea kukamilika baada ya wakala wake kukutana na wawakilishi wa FC PORTO kukamilisha miaka 25 ya kipa huyo kuichezea Real Madrid. Usajili ambao utawalazimu Real Madrid kumsajili David De Gea wa Man United.
Stoke City wameanza mazungumzo na kipa wa Aston Villa Shay Given kutaka kumsajili wakati huu ambapo kipa wao namba moja anawindwa na Chelsea na Man United.
Jonjo Shelvey amesaini mkataba mpya wa miaka minne kuichezea Swansea
Sevilla imekubali kumsajili kiungo wa Stoke City Mfaransa Steven Nzonzi kwa ada ya uhamisho paundi milioni 7.
Raheem Sterling amegoma kabisa kuichezea Liverpool na sasa analazimisha uhamisho ili kuondoka katika klabu hiyo. Taarifa zinasema kuwa katika mazoezi hajatokea na pengine sasa itawabidi Liverpool wakubali dau lililoletwa na Man City ili kumwondoa klabuni hapo.
Arsenal na Tottenham Hotspurs wameingia katika vita ya kumwania beki wa Roma Kostas Manolas ukitaka kujua uwezo wa beki huyu jaribu kutembelea youtube uone alichofanya msimu uliopita.
AC Milan imemwongezea mkataba wa mwaka mmoja beki wake mkongwe Philipe Mexes ambapo sasa atakaa katika klabu hiyo mpaka Juni mwaka 2016.
Real Madrid wanafikiria kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho ambaye amekua akiwaniwa kwa kiasi kikubwa na Man United na Arsenal. Real Madrid wanataka kumsajili Carvalho kama mbadala wa Asier Illarramendi
Olympic Lyon imewasajili wachezaji watatu kwa mpigo ambao wamejifunga mpaka mwaka 2020 ambao ni Antony Lopes, Nabil Fekir na Corentin Tolisso.
No comments