HENDERSON??!! MATTEO KOVACIC AU GUNDO WANGEKUFAA ZAIDI RODGERS



Huu ni wakati ambao timu mbalimbali barani ulaya zipo katika mchakato wa usajili wa wachezaji na mashabiki huwa na shauku kubwa sana ya kutaka kujua timu zao zitasajili wachezaji wa aina gani huku makocha wa timu hizo wengi wakiwa wanagongeana bilauri za mvinyo wa kifaransa na familia zao katika kipindi hiki cha majira kiangazi,mmoja wa makocha ambao nimeweka jicho langu kwake kwa sasa ni basi Brendan Rodgers ambaye katika kipindi cha mwaka mmoja sasa amepoteza mchezaji aliyetufanya tuamini yeye ni zaidi ya Wenger na Mourinho katika msimu wa 2013/14 Luis Suarez ambaye mpaka leo ameshindwa kuziba pengo lake kwa kuwasajili kina Lambert, Balotelli na sasa Danny Ings tukiwa katika wakati ule na majira yale yale tofauti ni kwamba sasa wamepoteza utii badala ya yale mabao murua ya Luis na kiongozi aliyekua anavalia jezi namba 8 kwa mara ya kwanza msimu unaokuja  tutaishuhudia Liverpool bila ya Steven Gerrard ambaye mchango wake kwa Liverpool umekua ni mkubwa kwa muongo mmoja na nusu..

Huyu ni mtu muhimu sana kwa The Kops kuliko kuliko mchezaji mwingine yeyote aliyecheza nae katika kipindi chake hadi hawa waliopo sàsa..mabao yake ya mita 40 na mapenzi yake kwa Liverpool yatamfanya aishi katika nyoyo za mashabiki wa timu hiyo kwa miaka mingi na huku wakimzungumzia zaidi kuliko dunia inavyomzungumzia Messi.



Timu chache sana hufanikiwa kuziba mashimo yanayoachwa wazi hasa katika sehemu ya kiungo yenye mchezaji wa kiwango cha Steve G' mfano mzuri Chelsea kuziba pengo la Lampard na Cesc au Barcelona kwa Ivan Rakitic kuchukuà nàfasi ya Xavi,hapa mashabiki wa Manchester United,Arsenal ni mashahidi mpaka leo Patrick Viera, Roy Keane na Paul Scholes wapo katika vinywa vyao kuliko hata Cristiano Ronaldo na Thierry Henry kuna wakati Zidane alimwambia Perez..

sisi ni sawa na gari nzuri ya kifahari ambayo ikikosa injini basi haiendi alikua akimzungumzia Makelele aliyekuwa mtumwa wa Galactico ya kipindi hicho ambaye aliuzwa katika klabu ya Chelsea baada ya kudai ongezeko la mshahara..Tatizo hili hili lililoitafuna baadhi ya timu kubwa kipindi cha nyuma natarajia kuliona Liverpool kwa muda kama Rodgers hatofanya maamuzi sahihi na kumtafuta mtu sahihi kwa wakati sahihi wa kuvaa viatu vya Steven G'.



Henderson ambaye Rodgers anamuamini hafikii hata robo ya uwezo wa Steve ambaye aliwafanya mashabiki wa timu hiyo kuishi nchi ya ahadi ambayo mito yake ilikua inatitirisha maziwa wakati huu ambao anawasajili kina Ings anatakiwa ajiulize viatu ambavyo Henderson's vilimpwelepweta hata wakati wa uwepo wa Steve ataviweza wakati huu ambao kiungo cha Liverpool kimebaki na Joe Allan na Lucas Leiva?! jibu ni hapana..Hendo ni mchezaji wa kuziba mianya zaidi si mchezeshaji kazi ambazo Gerrard alizifanya zote mbili hata baada ya kuondokewa na Mascherano na Alonso aliibeba timu yake kwa
miguu yake maridhawa kitu ambacho Jordan ataishia kukiota tu.



Dogo Matteo Kovaçic,Ever Banega au Ilkay Gundogan ambaye yupo sokoni hawa wote ni makondakta wazuri sana hasa nyuma yao wakiwa na mtu kama Hendo ambaye kazi chafu anaziweza pamoja na usajili mpya Milner..napenda kuiona Liverpool ikishindana ambayo kushoto yupo Firmino,kulia Milner au kinyume chake sio Sterling asiyejua thamani ya ile jezi nyekundu,Coutinho nyuma ya Lacazette au Sturridge, Hendo na Gundogan au Matteo kwenye kiungo..napata tu wasi wasi na nguvu ya ushawishi wa BR kwa wachezaji wazuri ikiwa alishindwa kusajili wachezaji wa maana akiwa na tiketi ya Uefa mkononi na fungu la kutosha baada ya kuuzwa Luis kwa sasa itakuaje.. tusubiri tuone ila hamu yangu ipo kwa atakayevaa viatu vya Steve G'8.

Zahir Bilali

No comments

Powered by Blogger.