TETESI ZA USAJILI KATIKA SOKA ULAYA LEO JUMANNE
Liverpool wako tayari Kumtoa mshambuliaji Rickie Lambert na pesa katika harakati zao za kumsaini mshambuliaji wa Aston Villa Christian Benteke. (Daily Mirror)
Arsenal wanasubiri mpaka kumalizika kwa michuano ya kombe la mataifa ya Amerika ili kutangaza kumsajili Artudo Vidal ambaye alihusishwa kujiunga na Man United mwaka jana
(Daily Star)
Kocha wa Man United Louis van Gaal amefunguka na kusema moja kati ya mikakati yake kwa ajili ya msimu ujao ni kummsajili kiungo Mkabaji na Ilkay Gundougan toka Borusia Dortmund anatajwa mno kujiunga na Mabingwa hao wa Kihistoria wa Ligi Kuu nchini England.
(Daily Express)
Mabingwa wapya wa England Chelsea wanaandaa kiasi cha paundi milioni 20 kumnasa mchezaji wa kimataifa wa Ghana Baba Rahman.
(Daily Star)
Baada ya kutemwa na Real Madrid meneja Carlo Ancelotti ameonekana kupewa kipaumbele katika kupata nafasi ya kuchukua mikoba ya kuifundisha West Ham baada ya kuondoshwa Sam Allardyce japokua taarifa zinasema Ancellot anachukua mapumziko ya mwaka mmoja nchini Canada
(Daily Telegraph)
Aliyekua kocha wa Dortmund Jurgen Klopp amepewa nafasi kubwa kuchukua kibarua cha kuifundisha Liverpool baada ya kutoka taarifa kuwa siku za kocha Brendan Rodgers pale Liverpool zinahesabika baada ya kipigo walichopata majogoo hao cha bao 6-1 toka kwa Stoke City
(Daily Mirror)
:::: TUKUTANE KESHO KWA HSBARI ZINGINE
No comments