STEVEN GERARD AAGWA KWA KICHAPO ANFIELD

Sherehe za kumuaga Nahodha wa Liverpool Steven Gerard zimeingia do baada ya kuchapwa bao 3-1 na Cystal Palace katika pambano la Ligi kuu Nchini England.

Mechi hiyo ya mwisho katika dimba la Anfield msimu huu ilikua mahususi kwaajili ya kumshukuru Nahodha Steven Gerard kwa utumishi uliotukuka wa miaka 17 akiwa na kikosi cha Liverpool.

Mechi ilianza kwa gwaride maalumu ambalo wachezaji wa Liverpool na Wale wa Crystal Palace walijipanga kumpigia makofi wakati Gerard akitoka katika vyumba vya kubadilishia akiwa ameongozana na wanae watatu.

MCHEZO WENYEWE

Pambano lilianza kwa kasi huku washambuliaji wa Liverpool wakiwa na nguvu zote kutaka kuongeza furaha kwa mashabiki waliofurika na kuujaza uwanja wa Anfienld na Philip Coutinho,Raheem Sterling na Adam Lallana.

Liverpool walitangulia kupata bao kupitia kwa Adam Lallana kabla ya Panchon hajasawazisha kwa mpira wa adhabu ndogo kama alivyowafanya Man United walipokutana katika dimba la Selhust Park wiki iliyopita hivyo kufanya mchezo huo kwenda mapumziko ukiwa ni sare ya 1-1.

Licha ya kosa kosa za hapa na pale ambazo washambuliaji wa Liverpool walizifanya Crystal Palace ndio walionekana kuwa makini na bora zaidi kipindi cha pili hasa Mcongoman Bolasie ambaye aliisumbua sana safu ya ulinzi ya Liverpool.

Goli la pili la Palace lilifungwa na Wilfried Zaha ukiwa ni mpira wake wa kwanza kuugusa akitokea benchi akiunganisha pasi ya Bolasie na dakika za mwisho Palace wakaongeza bao la tatu na la mwisho kupitia kwa Glenn Murray aliyeingia kuchukua nafasi ya Bolasie.

Mpaka mwisho wa mchezo Liverpool walilala kwa bao 3-1 na ndiyo mechi ya mwisho kwa Steven Gerarf katika uwanja wa Anfield kwani msimu ujao atatimkia USA.

.....

No comments

Powered by Blogger.