PEP GUADIOLA NA JARIBIO LA KUUA NDEGE WAWILI NA JIWE MOJA
..... Waswahili wana msemo wao maarufu wa mshika mawili moja humponyoka,ndicho ninachokiwaza hapa kuelekea marudiano ya nusu fainali ya klabu bingwa ulaya leo usiku kati ya wenyeji Bayern Munich dhidi ya Barcelona katika dimba la Alianz Arena jijini Munich, Germany huku wenyeji wakiwa na kazi ngumu ya kubadili matokeo na hatimaye kuvuka hatua inayofuata..
Pep Guadiola ni kocha anaefahamika zaidi na falsafa yake ya pasi fupi fupi na la kushambulia na kuitawala timu pinzani huku kila mchezaji akitakiwa kutimiza majukumu yake kwa wakati ili timu icheze vile atakavyo lakini kwa leo hali itakua tofauti uwezo wa timu yake kushambulia unatakiwa uwe sawia na ule wa ukabaji hasa watakapokuwa hawana mpira kwa kuwa wanacheza na timu ambayo na yenyewe inapenda kuwanyanyasa watu vilevile hapa nafananisha na sumaku zenye mwelekeo unaofanana zinapokutana wataalamu wa fizikia wanaelewa nasema nini..
Ili ngamia apite kwenye tundu la sindano Bayern itabidi ishambulie kama ilivyofanya Barcelona wakati fulani pale Camp Nou na Mourinho akala 5 wakati huo wanahitaji mbinu za kiitaliano na zile za Mourinho katika ukabaji na hili linataka nidhamu sio kama ile ya kushambulia ukiwa nyuma ya bao 2-0 aliyoitumia Pep na kufungwa bao la tatu katika mechi iliyopita..
Kuzuia Barcelona wasikufunge wakiwa na Messi, Neymar na Suarez ni sawa na wakazi wa bondeni kuyazuia maji kwa kuweka viroba..angelikuwa na Robben na Ribery leo Bayern ingekuwa katika sayari ya kipekee hawa wangewafanya Alba na Alves wasikimbie kilomita nyingi kwenda kushambulia wangewaza zaidi kuzuia hawa mapacha wawili na beki ya Barcelona huwa inafanya makosa mengi tu bila kuadhibiwa
Ikiwa Pep atafanikiwa na mbinu yoyote atakayoingia nayo leo usiku basi ataishangaza dunia ila bado nahofia yasije kuwa ya kuvuja kwa pakacha ikawa nafuu kwa mchukuzi
No comments