BARCELONA YATINGA FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA


Vinara wa ligi kuu nchini Spain FC Barcelona wamefanikiwa kutinga katika faibali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu baada ya kuwatoa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich ya kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-3.

Licha ya Barcelona kupoteza mchezo wa wake uliopigwa usiku wa jana kwa bao 3-2 lakini bado waliweza kuvuka hatua hii baada ya kuwa na faida ya magoli 3-0 waliyoyapata pale Nou Camp katika mechi ya awali.

Hii ni mara ya kwanza kwa Barcelona kufika Fainali tangu mwaka 2011 walipofika na kuchukua kombe.

Bayern walitangulia kupata bao la kwanza kupitia kwa Beki Benatia kwa kichwa kabla ya Neymar hajasawazisha na kuongeza bao la pili pasi zote za magoli zikitoka kwa Luis Suarez.

Mshambuliaji Roberto Lewandowski akafunga bao la pili na Thomas Muller akamalizia bao la tatu na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa bao 3-2 Bayern wakishinda na kumaliza ukame wa kukosa ushindi kwa mechi 3 mfulululizo.

Barcelona sasa inasubiri mshindi wa mechi ya leo kati ya Real Madrid na Juventus kucheza fainali Juni 4 pale Berlin.

  MAMBO MUHIMU KUYAFAHAMU BAADA YA MECHI YA JANA


  • Magoli mawili aliyofunga Neymar jana yanawafanya washambuliaji watatu wa Barcelona yani Messi,Suarez na Neymar kufikisha magoli 114 katika mashindano yote msimu huu: Messi magoli 53, Neymar magoli 37 na Suarez magoli 24.
  • Barcelona inaingia fainali ya nne tangu mwaka 2006 ikiwa na rekodi ya kuchukua kombe hilo katika fainali zote hizo tatu zilizopita yani mwaka 2006 wakiifunga Arsenal, Mwaka 2009 na 2011 walipoifunga Man United.
  • Bayern Munich walipiga mashuti 19 langoni mwa Barcelona hii ni rekodi kwa timu zilizowahi kucheza na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mwaka 2008 walipocheza dhidi ya Schalke 04.
  • Barcelona wamefika katika Fainali yao ya 18 katika ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ikiwa ni timu ya kwanza kufanya hivyo katika historia.
  •  Roberto Lewandowski amefunga magoli mengi zaidi akiwa amefunga magoli 22 tangu msimu wa 2012/2013 akiwa amezidiwa na Cristiano Ronaldo mwenye magoli 38 na Lionel Messi mwenye magoli 26.
  • Bayern Munich Jana wamefanikiwa kuwazuia Bayern Munich kufikia rekodi yao ya kushinda mechi 10 mfululizo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

~ Imetayarishwa na Edo Daniel Chibo

like page zetu na kutufollow
facebook: Wapenda  Soka-kanndanda
Instagram : @wapendasoka
twitter: @wapendasoka

No comments

Powered by Blogger.