MESSI APIGA BAO MBILI BARCELONA WAKIKABIDHIWA KOMBE NA KUMUAGA XAVI
Lionel Messi alifunga magoli mawili katika sare ya bao 2-2 waliyoipata Barcelona nyumbani Dhidi ya Depotivo la Coruna katika dimba la Camp Nou.
Ilikua mechi ya mwisho kwa Barcelona katika ligi ambapo walikabidhiwa pia kombe lao baada ya kuibuka mabingwa msimu huu.
Ilikua pia mechi ya kumuaga nguli wa timu hiyo Xavi Hernandez ambaye ameamua kuihama klabu hiyo na kuelekea Uarabuni.
Kwa Upande wa Depotivo imekua sherehe kubwa kwao kwani sare hiyo imewanusuru kushuka daraja.
No comments