HABARI FUPI PUPI ZA SOKA LEO ALHAMISI
■ Mbeya City wanaelekea kukamilisha usajili wa mchezaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars Haruna Moshi Boban kwa mkataba wa mwaka mmoja.
■ Aliyekua kocha wa Kagera Sugar Jackson Mayanja na msaidizi wake Mrage Kabange wameonyeshwa mlango wa kutokea huku uongozi wa timu hiyo ikitafuta kocha mwingine.
■ Mshambuliaji wa timu ya Mgambo JKT Malimi Busungu anafurahishwa na taarifa za kutakiwa na wekundu wa Msimbazi Simba SC na anakaribisha mazungumzo na klabu hiyo kongwe.
■ Wakali mbali mbali katika soka leo wanaadhimisha siku zao za kuzaliwa wakiwemo Kyle Walker (Tottenham) Alexender Lacazette (Lyon) na Charles N'zogbia (Aston Villa)
■ Shirikisho la Soka Duniani FIFA limepanga kuendelea na mchakato wa uchaguzi mkuu wa Rais Wa FIFA utakaofanyika kesho Ijumaa licha ya kukumbwa na kashfa nzito ya rushwa ambapo maofisa 6 wa ngazi ya juu wamekamatwa na polisi.
■ Mlinzi wa Chelsea Gary Cahill anakua mchezaji wa kwanza kushinda makombe yote makubwa na muhimu kwa kipindi kifupi katika historia ya soka la England. Tangu alipojiunga na Chelsea mwaka 2012 mchezaji huyo mwenye miaka 29 ameshinda Kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (2012), Europa League (2013), Capital Cup na Ligi kuu England (2015).
■ Sevilla jana imetetea ubingwa wa kombe la Europa wakiichapa Dnipro bao 3-2 na kujikatia nafasi ya kucheza katika ligi ya mabingwa barani Ulaya mwakani na kufanya klabu 5 kupata nafasi ya kushiriki kutoka katika nchi ya Spain ikiwa ni sheria mpya ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa bingwa wa kombe la Europa kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya.
NI HAYO TU KWA SASA TUKUTANE SAA 4 USIKU KUANGALIA HABARI ZOTE ZA USAJILI ZILIZOTIKISA VICHWA VYA WAPENDA SOKA LEO
Good
ReplyDeleteGood
ReplyDelete