MAN CITY YAISHUSHA DARAJA QPR KWA KIPIGO CHA BAO 6


Manchester City imeirudisha Queens Park Rangers katika ligi daraja la kwanza (Championship)baada ya kuishushia kichapo cha bao 6-0 mchezo wa ligi kuu Nchini England katika dimba la Etihad jijini Manchester.

QPR ambao ndiyo wamepanda na kucheza ligi kuu msimu huu baada ya kushuka misimu miwili iliyopita imejikuta inarudi ilipotoka na msimu ujao itaanza tena kampeni ya kutafuta nafasi ya kucheza ligi kuu.

QPR Imekua timu ya pili msimu huu kushuka daraja zikiwa zimebaki mechi 3 baada ya Burnley kushuka daraja pia siku ya Jumamosi na hii ni mara ya 5 QPR wanashuka daraja kutoka katika ligi kuu nchini England wakishuka pia mwaka 1969,1979, 1996, 2013.

Man City walipata magoli yao kupitia kwa Sergio  Agüero aliyefunga magoli matatu peke yake na magoli mengine yakifungwa na Kolorov,James Milner na David Silva.

Magoli matatu ya Aguero leo yanamfanya kuwa ameshafunga magoli 6 katika mechi mechi 4 zilizopita dhidi ya QPR Na ameweka rekodi katika klabu yake ya Manchester City kwa kufunga magoli 24 katika msimu mmoja wa ligi kuu akivunja Rekodi ya Tevezi msimu wa 2009/2010 na ile yake mwenyewe aliyoiweka 2011/2012.

Sergio Agüero pia amefunga hat trick yake ya pili katika msimu huu baada ya kuifunga Tottenham bao 4 mwezi Oktoba mwaka 2014.

JE TIMU IPI ITAUNGANA NA BURNLEY NA QPR KUSHUKA DARAJA MSIMU HUU?

No comments

Powered by Blogger.