CHELSEA NA LIVERPOOL HAKUNA MBABE
Mabingwa wa ligi kuu nchini England Chelsea wamelazimishwa sare na wenyeji Liverpool katika mechi ya ligi kuu jioni hii.
Mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Stamford Bridge jijini London ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 John Terry akitangulia kufunga kwa kichwa kwa upande wa Chelsea akiunganisha mpira wa kona kisha nahodha wa Liverpool Steven Gerard akasawazisha dakika chache kabla ya mapumziko na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko matokeo yakiwa ni bao 1-1.
Kipindi cha Pili Liverpool watajilaumu wenyewe baada ya Philip Countinho kukosa nafasi mbili za wazi ambazo pengine zingebadilisha matokeo ya mchezo huo.
Vitu vikubwa viwili vilionekana katika mchezo wa leo kwanza Gwaride rasmi kwa mabingwa wapya Chelsea ambapo Liverpool walijipanga kuwapongeza Chelsea kabla ya mchezo huo na tukio lingine lilikua mashabiki wote katika uwanja kusimama kumpigia makofi nahodha wa Liverpool Steven Gerard alipokua akitoka uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Lucas Leiva.
Kwa matokeo hayo Liverpool wameendelea kujiimarisha katika nafasi ya 5 baada ya Tottenham kupoteza mchezo wake jana.
No comments