LIVERPOOL YAKUMBANA NA KIPIGO KIZITO MECHI YA MWISHO. HULL CITY YASHUKA DARAJA


Pazia la Ligi kuu nchini England limekamilika leo kwa mechi 10 kuchezwa katika viwanja tofauti huku matokeo ya kushangaza yakipatikana katika mechi hizo.

Liverpool wakisafiri mpaka jijini Stoke walikumbana na kichapo cha hatari cha bao 6-1. Arsenal wao wakiwa nyumbani waliilamisha West Brom bao 4-1. Chelsea ambao ni mabingwa walinogesha ubingwa wao kwa kuwafunga Sunderland bao 3-1.

Kwa ufupi jumla ya magoli 29 yamefungwa katika mechi zote 10 zilizopigwa leo Stoke City,Leicester City na Arsenal wakiongoza kwa kufunga magoli mengi wakiwa wamefunga magoli 15 kwa pamoja.

Hull City imeshuka daraja baada ya kushindwa kupata ushindi katika mechi yao dhidi Man United huku Newcastle wakiibuka na ushindi wa bao 2-0 ushindi ambao waliuhitaji vilivyo kuweza kubaki katika ligi kuu.

Chelsea ambao ni mabiwa walikabidhiwa kombe baada ya kuwalaza Sunderland bao 3-1
Hivyo basi Chelsea,Man City,Arsenal na Man United wamepata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Ulaya wakati QPR,Burnley na Hull City wameshuka daraja

YAFUATAYO NI MATOKEO NA WAFUNGAJI KATIKA MECHI ZOTE ZA LEO.


ARSENAL 4-1 WEST BROM

- Theo Walcot (4',15',37')
- Jack Wilshere (17')
Gareth McAuley ( 57')

ASTON VILLA 0-1 BURNLEY

- Danny Ings (6')

CHELSEA 3-1 SUNDRLAND

- Sten Fletcher (26')
- Diego Costa (37')
- Loic Remy (70',88')

CRYSTAL PALACE 1-0 SWANSEA 

- Marouane Chamakh (57')

EVERTON 0-1 TOTTENHAM

- Harry Kane (25')

HULL CITY 0-0 MAN UNITED


LEICESTER CITY 5-1 QPR

- Jamie Vardy (16')
- Marc Albrighton (43')
- Ulloa (51')
- Cambiasso

MAN CITY 2-0 SOUTHAMPTON

-Frankie Lampard (31)
Sergio Aguero (88')

STOKE CITY 6-1 LIVERPOOL

- Dioudf (22', 26')
- Walters (30')
- Charlie Adam (41')
- Nzonzi (45')
- Peter Crouch (86')

No comments

Powered by Blogger.