HAYA NDIYO MAAFA YALIYOLETWA NA MASHABIKI WA LIVERPOOL MIAKA 30 ILIYOPITA
Tarehe kama ya leo Miaka 30 iliyopita Michel Platin ambaye ni Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) alifunga goli pekee kwenye Fainali ya Kombe la Europa (EUROPEAN FINAL CUP) kati ya Liverpool na Juventus ilikua ni tarehe 29 May 1985.
Fainali iliyofanyika katika jiji la Brussel Ubelgiji katika uwanja wa Heysel ambapo mashabiki 39 walikufa na wengine 600 baada ya kuangukiwa na ukuta wa uwanja huo uliobomoka kufuatia mashabiki wa Juventus kujaribu kuwakimbia mashabiki wa Liverpool waliovunja uzio unaotenganisha baina ya mashabiki katika uwanja na kuanza kuwafata mashabiki wa Juventus ili kuwafanyia fujo na katika harakati za kuokoa maisha yao ndipo walipoangukiwa na ukuta huo na kupoteza maisha.
Kati ya mahabiki waliokufa siku hiyo 32 walikua ni Wataliano, wanne Wabelgiji, wawili wafaransa na mmoja ni kutoka Ireland ya Kaskazini.
Licha ya maafa hayo mchezo uliendelea na Mchezaji bora wa dunia wakati huo Michel Platin alifunga goli pekee katika mchezo huo ambapo Juventus waliibuka kuwa wababe wa Ulaya.
Kutokana na tukio hilo hilo timu zote kutoka England zilisimamishwa kushiriki michuano yote ya Ulaya kwa miaka mitano huku mashabiki 14 wa Liverpool wakihukumiwa vifungo vya miaka mitatu jela.
~ Edo Daniel Chibo
No comments