HABARI FUPI FUPI ZA SOKA ZILIZOTAWALA LEO IJUMAA
● Aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Kim Paulsen ni mmoja kati ya makocha wanaopewa nafasi ya kuchukua nafasi ya kuifundisha klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam
● Rais Wa FIFA Sepp Blatter amechaguliwa kwa mara ya Tano kuliongoza shirikisho hilo linalosimamia soka dunia na hii itamweka tena madarakani mpaka mwaka 2019 ambapo ametangaza kuwa hiki kitakua ni kipindi chake cha mwisho kugombea Uongozi katika FIFA.
● Michuano ya Kombe la soka kwa mataifa ya Bara la Amerika Kusini yataanza kutimua vumbi tarehe 11 Juni katika nchi ya Chile ambapo wenyeji Chile watacheza na Ecuador.
Michuano hiyo itadumu mpaka tarehe 4 June na itashirikisha timu 10 za bara la America ya Kusini pamoja na Mexico na Jamaica huku bingwa mtetezi akiwa ni Paraquay.
● Timu ya taifa ya soka ya Malawi imetawazwa kuwa kuwa mabingwa wapya wa kombe la COSAFA baada ya kuwafunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa fainali nchini Afrika Kusini.
● Timu iliyopanda daraja katika ligi kuu Nchini England AFC Bournemouth imetangaza kumsajili mchezaji wa kimatifa wa Ghana anayekipiga Chelsea Christian Atsu kwa mkopo wa msimu mzima.
● Southampton wamekataa dau la paundi milioni 10 ambalo Liverpool waliitoa katika juhudi za Kumsajili mlizi wa timu hiyo Nathaniel Cylne ambaye ametajwa kwa muda mrefu kuwaniwa na Manchester United.
~ Edo DC
No comments