ARSENAL YAWEKA REKODI YA AINA YAKE KOMBE LA FA
Arsenal imekua timu ya kwanza kushinda kombe la FA mara nyingi zaidi baada ya kushinda kwa mara ya 12 Ikiifunga Aston Villa bao 4-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa katika dimba la Wembley jijini London.
Arsenal wameweza kutetea ubingwa wao walioshinda mwaka jana wakiifunga Hull City bao 3-2.
Ushindi wa Arsenal leo haukua na mashaka kwani waliwatawala vilivyo Aston Villa na kufanikiwa kupata magoli yake kupitia kwa Theo Walcot, Alexis Sanchez, Per Metasacker na Olivier Giroud na kuzima kabisa matumaini ya Aston Villa waliotaka kuchukua kombe hilo mara ya kwanza baada ya kulikosa kwa miaka 15 iliyopita.
Goli alilofunga Alexis Sanchez leo linamfanya kuwa mchezaji wa pili kutoka Chile kufunga katika fainali baada ya kutanguliwa na George Robledo wa Newcastle United mwaka 1952.
No comments