YANGA, ETOILE ZAINGIZA MIL 223

Mchezo no.91 wa Kombe la Shirkisho
barani Afrika (CC) hatua ya 16 bora
uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini
Dar es salaam, kati ya wenyeji timu ya
Young Africans dhidi ya Etoile du Sahel
kutoka Tunisia umeingiza jumla ya sh.
223,135,000.

Jumla ya watazamaji 36,105 walikata
tiketi kuhudhuria mchezo huo, huku VIP
A zikikatwa tiketi 68, VIP B tiketi 869,
VIP C tiketi 582, Orange tiketi 1,955 na
viti vya rangi ya Bluu na Kijani tiketi
32,631 ziliuzwa.

Mgawanyo wa mapato ni VAT 18% sh.
34,037,542.37, Gharama ya tiketi sh.
11,462,000, Gharama ya Uwanja 15%
sh. 26,645,318.64, Gharama za mchezo
15% sh. 26.645,318.64, CAF 5% sh.
8,881,772.88, TFF 5% sh. 8,881,772.88
na Young Africans 60% sh.
106,581,274.58.

No comments

Powered by Blogger.