BAYERN MUNICH YAFANYA MAUAJI YA HATARI
Mchezo huo wa hatua ya robo fainali ulipigwa katika dimba la Alianz Arena jijini Munich ambapo Bayern Munich walitakiwa kushinda zaidi ya goli mbili ili wavuke hatua hii na mpango huo ulifanikiwa licha ya kuwakosa Arjen Robben na Frank Ribbery kikosini.
Thiago Alcantara alifungua karamu ya magoli kwa kufunga bao la mapema kabisa ambalo lilifungua milango ya mabao mengine ambayo Roberto Lewandoski alifunga mabao mawili, mlinzi Jerome Boateng akafunga moja,Thomas Mueller akafunga moja na kiong Javier Alonso akifunga bao la mwisho.
FC Porto ambao walionekana kupotea mchezoni waligunga bao lao kupitia kwa Nahodha Jackson Martinez bao ambalo halikusaidia kutowatupa nje ya michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo Bayern Munich wameibuka na ushindi wa jumla wa bao 7-4 na kuna uwezekano wakakutana na Barcelona hatua inayofata.
No comments