THE GUNNING MACHINE : POINTI 4 NYUMA YA CHELSEA, TUWAZE UBINGWA?

Na Richard Leonce Chardboy.

Ushindi mgumu wa bao 0-1 dhidi ya Burnley katika uwanja wa Turf Moore unaisogeza Arsenal mahali salama katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Akicheza mchezo wake wa 150 wa ligi, Aaron Ramsey akafanikiwa kufunga bao hilo muhimu na la kipekee katika mchezo huo.
Kuwa nyuma ya Chelsea kwa pointi nne kumewafanya baadhi ya watu waanze kuzungumzia kurejea kwa Arsenal katika mbio za ubingwa.

Kimsingi katika hesabu za mpira kitu hicho kinawezekana, japo hupaswi kusahau kwamba Chelsea wanaoongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 70 wana michezo miwili nyuma ya Arsenal ambayo kama wakipata pointi 6 basi watakua wametangulia kwa pointi 10.

Je, mbio za ubingwa kwa Arsenal zipo hai ukizingatia kasi ya Chelsea kwa msimu huu?

Unaweza kufanya hivi,
Iangalie ratiba yenyewe ya ligi ilivyokaa. Muda mchache kutok hivi sasa, Chelsea watakua ugenini kupambana na QPR ambao hawapo katika nafasi nzuri kwenye msimamo (wanaweza kutoa walichokitoa Burnley kwa Arsenal hapo jana au zaidi).
Baada ya mchezo huo, wakati Arsenal wakicheza na Reading katika nusu fainali ya kombe la FA April 18 Chelsea wao watakua nyumbani kuwakaribisha Manchester United ambao wanaifukuza Arsenal kwa karibu sana hivi sasa, na kama watapata matokeo mazuri leo hii dhidi ya Manchester City watakua na pointi 65. hivyo watahitaji ushindi tu dhidi ya Chelsea ili wakae juu ya Arsenal.

Lakini kitu cha kusisimua ni kwamba Arsenal watakaporejea kwenye ligi April 26, watawakaribisha Chelsea. kama hesabu zitakua mbaya kwa Chelsea katika moja kati ya michezo yake miwili ijayo, basi kuna uwezekano wa Asenal kuyageuza mambo iwapo tu watafanikiwa kuwafunga Chelsea katika mchezo huo.

Jambo muhimu kwa Arsenal ni kuhakikisha wanashinda michezo yao yote, ubingwa haupo mikononi mwao kabisa. Ubingwa upo mikononi mwa Chelsea lakini lolote linaweza kutokea.

Lakini pia iwapo Arsenal watateleza, wanaweza kujikuta katika nafasi mbaya sana kwa sababu Manchester United na Manchester City wanawafukuzia kwa kasi sana.
Wakati huu ni wakati wa kushika zaidi ulicho nacho, na kuwaacha wenzako wapigane katika njia zao.

Asante sana kwa muda wako.
Instagram: chardboy77
facebook: Richard Leonce Chardboy
Whatsapp: 0766399341
Email: chardboy74@ gmail
com

No comments

Powered by Blogger.