REAL MADRID YAUA 9-1 RONALDO APIGA BAO 5
Cristiano Ronaldo ameonyesha umwamba wake baada ya kufunga goli 5 peke yake ikiwa pia hat trick ndani ya dakika 8 tu wakati Real Madrid walipoibamiza Granada bao 9-1.
Wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo uliopita katika ligi dhidi ya Barcelona Real Madrid waliingia katika mchezo wa leo wakiwa na hamasa ya kurudi katika hali yake ya ushindi.
Gareth Bale alitangulia kuifungia Real Madrid ambao ni mabingwa wa Ulaya kwa bao la dakika ya 20 ya mchezo. Ronaldo akafunga bao la pili dakika ya 30 na kuongeza la tatu dakika 6 badae kabla ya kufunga bao lake la tatu na la nne kwa Madrid dakika ya 38 na kufanya mchezo huo kuwa 4-0 mpaka Mapumziko.
Baada ya kipindi cha Pili kuanza Benzema aliongeza bao la 5 kwa Madrid dakika ya 52 kabla ya Ronaldo kufunga bao la 6 kwa Madrid dakika Mbili baadae kisha Benzema akaongeza bao lingine na kufanya yafike 7 dakika mbili baada ya Ronaldo kufunga.
Granada ambao walionekana kuchanganyikiwa jinsi magoli yalivyoingia katika lango lao walijifunga dakika ya 83 kabla ya Ronaldo kumalizia bao lake la 5 kwa kufunga dakika ya 89. Granada walipata bao la kufutia machozi dakika ya 74 likifungwa na Ibanez.
MUHIMU KUIJUA HII
● - Magoli matano aliyofunga Ronaldo leo ni mara yake ya kwanza kufunga magoli mengi hivyo katika mechi moja.● Ronaldo amekua mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga goli 5 katika mechi moja katika Laliga Tangu mwezi mwaka 2002 wakati Fernando Morientes alipofunga bao 5 peke yake dhidi ya Las Palmas.
● Ronaldo sasa amemfikia gwiji wa zamani wa Real Madrid Alfred Di Stefano kwa kufikisha hat trick 28 katika historia ya Real Madrid.
● Hiki ni kipigo cha kwanza kikubwa kwa Granada tangu ilipoanzishwa.
● Ronaldo sasa amefikisha jumla ya Hat trick 24 katika La Liga sawa na Lionel Messi.




No comments