KWA HALI HII TUNAHITAJI KURUDI DARASANI KUJIFUNZA JINSI YA KUTOFAUTISHA ABJADI NA KONSONANTI.


Kuna msemo mzuri wa mababu zetu waliwahi kutuachia unaosema "Ulipendalo hupati , hupata ujaliwalo" . Ukibahatika siku moja kuingia kwenye viwanja vya mpira wa miguu hata kwenye ligi ya mchangani ambapo mchezaji hucheza na kiatu kilichotoboka kwa mbele na soksi yake chafu ikiwa imetokea kwa mbele utagundua ni watu wengi sana wanapenda mchezo huu tena kwa dhati, utakuta umati  mkubwa wa watu wakishangalia , ila ukiwaangalia vizuri huku tabasamu lako likiwa limejengeka usoni lazima unyong'onyee ghafla pindi ukumbukapo ule msemo "Ulipendalo hupati, upata ujaliwalo" .Mashabiki hawa wanaopigwa na jua, mvua wameacha kazi zao kuja kuangalia kitu wanachokipenda lakini hakuna kitu wanalichowahi kukipata kizuri zaidi ya malumbano ya viongozi na vitu vingine vibovu ambavyo wamejaliwa, ama hakika MUNGU kawajalia hawa mashabiki huzuni katika furaha yao.

Na huzuni hii katika michezo imesababishwa na wenye dhamana kwenye tasnia hii kushindwa kutofautisha Abjadi na Konsonanti, Hata kutofautisha kati ya Tonga na Tuwi kumetushinda, na tumebakia kuwa watu wenye huzuni siku zote kwenye kitu tunachokipenda, tumebaki kusubiri mtu atakayekuja kukamilisha ule msemo usemao "Nia njema ni tabibu".

Kwa mwaka jana 2014 tulikuwa na mawakala watatu tu wa mpira miguu John Ndumbaro, Mehdi Remtulla na Ally Saleh kutoka Zanzibar hii ni baada ya leseni ya Daniel Ndumbaro kuisha mwaka juzi na kukataa kuchukuwa leseni mpya baada ya kukatishwa tamaa na wachezaji wetu aliokuwa anawatafutia timu na baada ya mtu mfupi wanarudi bila sababu za msingi mfano, Jerry Tegete,Haruna Moshi, Joseph Kaniki ambao wote walipelekwa nchini Sweeden na wakarudi nyumbani bila sababu ya msingi, nahisi hata wale vijana kumi wakina Ndemla waliopelekwa Ujerumani na wakarudi wote nyumbani waliiendeleza filamu ya kina kaka zao  iliyokuwa sehemu ya kwanza. Imefikiwa wakati wachezaji wetu kujitafutia timu wenyewe nje, mfano kuna habari niliwahi kuzisikia mchezaji Jumanne Ramadhani aliwahi kwenda Bulgaria kutafuta timu na alishindwa kufanikiwa.Hivi ni lini tutapata mawakala wengi wenye nia njema kama ya Jorge Paulo Agostinho Mendez? .Ni lini tutapata wachezaji wenye nia ya dhati ya kuchezea nje? .Hapa jibu ni rahisi,Siku tukijua kutofautisha Abjadi na Konsonanti .


Viwanja vingi tunavyotumia leo hii havina tofauti na viwanja waliotumia wazee wetu miaka ya nyuma, Jezi tunazovaa leo hii ni zile zile alizowahi kuvaaTenga wakati anacheza mbele hazina nembo ya mdhamini yoyote.Mabango yaliyopo uwanjani ni yale yale ya miaka yote.Kweli tumekosa mtu mwenye nia njema?. Mtu wa kulifanya soka letu kuwa biashara kubwa? .Hakuna anayejua Sekta hii huingiza hela nyingi baada ya Sekta ya mafuta?  Viongozi wetu wamegeuza mpira kuwa ni taasisi ya kujiingizia hela. Ni wachache sana wenye nia njema na mpira wetu ambao wanaamini kupitia weredi zaidi. Imefika wakati vilabu vyetu viwe na viwanja vyao, viwe na wadhamini wengi ili kujiongezea vipato, mfanyabiashara huja sehemu yenye miundombinu mizuri. Jiulize ni vilabu vingapi vina GYM yao? Vipi kuhusiana na Zahanati ? kila siku tutaendelea kusikia habari za mchezaji kupata majeraha na kupewa likizo ya kwenda kujitibu kwao .

Kuna wakati umefika tumelingana na babu zetu wa zamani waliokuwa wanadanganyishiwa shanga kwa dhahabu.Jiulize kiko wapi kile kizazi cha Copa Coca Cola kilichokuwa mabingwa kule Brazil? Kwanini Rafaeli alienda Manchester united afu sisi tulishindwa kupeleka hata mchezaji mmoja Kaizer Chiefs, Tuachane na habari za kuwauza nje, hivi ni kweli kile kizazi cha dhahabu tumekitelekeza na kuking'ang'ania kizazi hiki cha shanga tulichonacho timu ya Taifa? Kwa kizazi kile kama tungekitunza ile ndoto yetu ya kushiriki AFCON ingetimia.

Wakati Rwanda ikianzisha ligi ya vijana wa umri wa chini ya miaka 15 na kuweka mazingira mazuri ya ligi, Kuanzisha vituo vingi vya vijana kwa lengo la kwenda Afcon 2019 sisi tunahangaika na bonanza la wiki mbili la Uhai Cup, Copa coca cola afu hatuna angalau vituo bora vya michezo vya kuwafunza vijana wadogo na tunategemea kwenda AFCON 2019 acha niwe na imani Taifa Starz mabolesho itatupeleka AFCON 2019, Tena kwenye nchi yetu hii inayoamini kupitia ushirikina kuliko mazoezi.Habari za Yanga na Simba kugomea kuingia kwenye vyumba vya kubadilisha nguo si habari ngeni tena wanaamini kuingia uwanjani kwa kuruka ukuta ni silaha tosha ya ushindi.Kweli tunahitaji wa kututofautishia kati ya ABJADI na KONSONANTI.

Wakati TFF inajitoa kwenye uwendeshaji wa ligi na kuiachia Bodi ya ligi.Pia ikavitaka vilabu baadhi ya viongozi kuajiliwa kulingana na Taaluma yake nilipata furaha kubwa niliona kweli ule weredi tuliokuwa tunauzungumzia umeanza kutekelezwa.Nilitegemea Bodi ya ligi ingekuja na faida kubwa , nilitegemea bodi ya ligi kuifanya ligi kuu kuwa bidhaa kubwa na bora wakati huo TFF wakiwa wamepunguziwa mzigo na kuendelea kufanya kazi za kukuza mpira wa miguu nchini lakini mategemeo yangu yalikuwa tofauti kabsaaa.Kichefu chefu zaidi huwa nakipata pale Masau bwire, Tobiasi Kifaru , Jerry Muro na maAfisa habari wa vilabu vyetu kugeuka kuwa makocha.Usitegemee kusikiliza kipindi cha mchezo leo hii , kesho Simba na Yanga wanacheza Afu ukategemea makocha wa Simba na Yanga kuwasikia wakizungumzia mbinu za mchezo wao ujao, Masikio yako yaandae kumsikiliza Muro na Manara . Mpira wetu unaendeshwa hivo hivo tu weredi upo mdomoni lakini siyo kwenye vitendo.

Tena usije ukategemea hili suala la Hajib na Banda ndo likawa tukio la mwisho, hapo kabla nilishawahi kushuhudia kwa macho yangu tukio kama hilo kwenye mazoezi ya JKT ORJOLO kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume hapa Arusha.Tumewakuza wachezaji wetu kwenye mazingira ya migogoro ndani ya vilabu vyetu hivyo usishangae kuwaona wakirushiana makonde kwenye mazoezi kwa sababu walishawahi kunywa damu ya ugomvi wakati wakiwa wanakuwa.
Hata mikataba wanayosaini mwisho wake ni ugomvi tu kwa hiyo usishutuke suala la Hassan Kessy , Kina Okwi, Juuko Murshid, Sserunkuna wanaishi hotelini .Wanaigharimu Simba kiasi cha shillingi milioni 15 kwa mwezi kiasi ambacho kinatosha kuwapangishia Wote wanne na Kessy watano nyumba na wakaishi vzuri.

Ama kweli elimu ya kutofautisha ABJADI na KONSONANTI inahitajika sana .

Asanteni.

Leo mchana nitawapa sababu za kwanini Arsenal atashinda dhidi ya liverpool na kwanini liverpool atashinda dhidi ya Arsenal.

#Martin kiyumbi.

Contact: 0657771077

No comments

Powered by Blogger.