LIVERPOOL ON FRIDAY : ARSENAL VS LIVERPOOL MAMBO UNAYOPASWA KUYAJUA
Leo katika LIVERPOOL ON FRIDAY tunaangalia kwa Undani pambano kati ya Liverpool watakaosafiri mpaka jijini London kuivaa Arsenal katika uwanja wa Emirates.
Awali ya yote mwana Liverpool unapaswa kufahamu kuwa Winga na Mshambuliaji Raheem Sterling amegoma kusaini mkataba mpya na ametaka mazungumzo juu ya mkataba wake yazungumzwe baada ya msimu kuisha.
Sterling amekataa kusaini mkataba utakaompa Paundi laki moja kwa wiki ili aongeze mkataba wake baada ya ule wa sasa kumalizika mwishoni mwa msimu ujao na kuzidisha tetesi za yeye kutaka kuihama Liverpool huku vilabu kadhaa vikihusishwa kumwania nyota huyu ambaye huichezea pia timu ya taifa ya England.
ARSENAL VS LIVERPOOL
Sasa tuje katika pambano la Jumamosi hii kati ya Arsenal na Liverpool katika dimba la Emirates.
Baada ya kupoteza mechi dhidi ya Man United Liverpool iko tayari kupokea mtihani mwingine dhidi ya timu ambayo haitabiriki ya Arsenal.
Arsenal wanaweza kukosa huduma ya mshambuliaji Danny Welbeck ambaye alipata matatizo ya goti akiitumikia timu ya Taifa ya England
Mikel Arteta, Alex-Oxlade Chamberlain, Mathieu Debuchy na Abou Diaby wote walikua mazoezini Ijumaa lakini hakuna uhakika kama watakua fit kucheza.
Liverpool watakosa huduma ya Steven Gerrard na Martin Skrtel ambao wanaanza kutumikia adhabu zao za mechi tatu huku Lucas akirudi kikosini akitokea majeruhi
Daniel Sturridge, Raheem Sterlin na Adam Lallana wote hao wanasubiri ripoti ya daktari ili wacheze baada ya kuwa majeruhi.
Nafasi kubwa msimu huu sio ubingwa bali ni kugombania nafasi ya kucheza Ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao. Chelsea,Man City, Arsenal, Man United,Liverpool na Tottenham zote zinawania nafasi nne za juu ili kucheza katika ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.
MAMBO MUHIMU YA KUYAFAHAMU
Arsenal wamepoteza mchezo mmoja tu katika michezo 7 waliyocheza dhidi ya liverpool wakishinda mara 4 na kutoka sare mara 2 wakati Liverpool imeshinda mechi moja tu katika mechi 18 walizocheza dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates wakitoka sare mara 7 na kupoteza mara 10 katika mashindano yote.
Mara ya mwisho kwa Liverpool kushinda katika uwanja wa Emirates ilikua mwezi Agosti mwaka 2011 na pambano kati ya Arsenal na Liverpool limevunja rekodi kwa kua pambano lililozalisha Hat Trick Nyingi zaidi (Hat trick 5) katika ligi hakuna pambano lolote lililoweza kufikia rekodi hii
Arsenal imeshinda mechi moja tu nyumbani kwao Emirates dhidi ya timu zilizo katika nafasi 5 za juu katika msimamo wa ligi kuu Nchini England msimu huu yani Chelsea,Man City, Man United na Liverpool na hii ni katika mechi 11 zilizopita.
Katika mechi 16 Arsenal imeshinda mechi 14 tangu kuanza kwa mwaka huu 2015 ikiwa pia ni ushindi mara 9 katika mechi 10 za ligi ambazo wamecheza huku wakivunja rekodi ya kutopoteza mechi 8 mfululizo katika mechi za zilizopigwa Emirates.
Kama Liverpool itashinda bila kufungwa basi itajiwekea rekodi yake klabuni hapo kwa kushinda bila kufungwa goli lolote katika mechi 7 za ugenini baada ya kufikia rekodi ya mwaka 1966 na 1972
Liverpool imeshavuna pointi 26 katika ligi kwa mwaka huu ikizidiwa na Arsenal waliopata pointi 27 mwaka huu 2015.
---____________________________
Weekend Njema

No comments