JUVENTUS MGUU MMOJA NDANI NUSU FAINALI MABINGWA ULAYA


Mabingwa wa Italia klabu ya Juventus toka jiji la Turin nchini Italia jana walianza vyema hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya kuwabamiza Monaco bao 1-0.

Goli pekee katika mchezo huo lilifungwa kwa njia ya penati na kiungo Artufo Vidal baada ya Kuangushwa katika eneo la hatari na beki wa Monaco Calvalho.
Juventus wameendeleza rekodi yao ya kutofungwa na timu yoyote toka Ufaransa katika dimba lake la nyumbani.

Matokeo ya jana yanawaweka Juventus mguu mmoja ndani kuingia nusu fainali kwani watahitaji sare yoyote katika mechi ya marudiano wiki ijayo ambapo wakifanikiwa kuvuka itakua mara ya kwanza Tangu mwaka 2003 watakua wameingia katika nusu fainali.

++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.