ATLETICO MADRID NA REAL MADRID HAKUNA MBABE.
Mechi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya Robo fainali kati ya mahasimu wa jiji la Madrid Atletico Madrid na Real Madrid imemalizika kwa sare ya bila kufungana.
Pambano hilo lilipigwa katika dimba la Vicente Calderon nyumbani kwa Atletico Madrid ilikua ukumbusho wa mechi ya fainali ya michuano hiyo msimu uliopita wakati Real Madrid walipoibuka na ubingwa.
Pambano la jana Kila timu ilikua na munkari wa kupata ushindi la kila uimara wa magolikipa uliwanyima nafasi washambuliaji Cristiano Ronaldo,Benzema na Bale kwa upande wa Real Madrid na Torres , Mandzukic na Griezman kwa upande wa Atletico Madrid.
Mechi ya Marudiano itapigwa wiki ijayo katika dimba la Santiago ambapo Real Madrid watatakiwa kushinda ili kuvuka hatua hii wakati Atletico wao watahitaji sare tu ya Magoli ili kuingia Nusu fainali.

+++++++++++++++++++++++++++



No comments