HAPATOSHI LIGI KUU TANZANIA BARA LEO NA KESHO



Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea leo jioni  kwa michezo mitatu, mjini Morogoro wenyeji Polisi Morogoro watawakaribisha Ndanda FC kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Jijini Mbeya wenyeji timu ya Mbeya City watawakaribisha timu ya Simba SC kwenye uwanja wa Sokoine , huku Azam FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Chamanzi Complex.

Jumapili Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itaendelea  kwa maafande wa timu ya Ruvu Shooting  kuwakaribisha maafande wenzao wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Mabatini - Mlandizi, huku jijini Mbeya wenyeji timu ya Prisons FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar.

+++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.