LIVERPOOL ON FRIDAY : WAKALI HAWA NDIYO WATAKAOCHEZA TEAM GERARD VS TEAM CARRAGHER
Na : Edo DC
Ijumaa hii katika LIVERPOOL ON FRIDAY tunawaletea maelezo kuhusu mchezo wa Jumapili katika Dimba la Anfield ambapo wakongwe wa Liverpool ambao wameichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa hapa nawazungumzia Steven Gerard na Jamie Carragher watakua uwanjani kuviongoza vikosi vyao kucheza mechi ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya mahitaji kwa wasiojiweza na shukrani kwa Liverpool.Ni wakati mwingine ambapo dunia itawashuhudia Steven Gerrard,Luis Suarez, Thiery Henry na Fernando Torres katika timu moja
Wachezaji Steven Gerrard na Jamie Carragher ni wachezaji wenye historia kubwa katika klabu ya Liverpool na watatumia mechi hiyo kuwaaga rasmi mashabiki wao hasa Steven Gerard ambaye huu ni msimu wake wa mwisho kuichezea Liverpool wakati Jamie Carragher yeye alishastaafu na sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo cha SKY SPORTS.
Mpaka leo Ijumaa tiketi za kuingia katika mechi hiyo zilishaisha na mechi hii imeandaliwa na Liverpool foundation na inategemewa kutengeneza kiasi cha Paundi 500,000 na pesa hizo zitatumika kwa ajili ya kusaidia Alder Hey Hospital, Nyumba ya kulelea watoto ya Claire House na Vituo vingine zaidi ya 56 vya watoto wasiojiweza
WACHEZAJI WATAKAOCHEZA KATIKA MECHI HIYO
STEVEN GERARD
- Brad Jones: Kipa wa Liverpool
- John Terry: Nahodha wa Chelsea
- Stephen Warnock: Mchezaji wa zamani wa Liverpool anayeichezea Derby County hivi sasa.
- Scott Dann: Mlinzi wa Crystal Palace
- Ashely Williams: Nahodha wa Swansea
- John Arne Riise: Mchezaji wa Zamani wa Liverpool na anaichezea APOEL hivi sasa
- Anthony Gerrard: Mjomba wake Steven Gerard na ni mchezaji wa Oldham Athletic
- Steven Gerrard: The man himself (Muhusika mkuu)
- Kevin Nolan: Nahodha wa West Ham
- Charlie Adam: Kiungo wa Stoke City midfielder na mcheza wa zamani wa Liverpool
- Jay Spearing: Mchezaji wa Blackburn Rovers ambaye aliichezea Liverpool zamani kama kiungo
- Xabi Alonso: Kiungo wa zamani wa Liverpool anayeichezea Bayern Munich.
- Ryan Babel: Mshambuliaji wa Zamani wa Liverpool anayeichezea Kasimpasa hivi sasa
- Thierry Henry: Nahodha wa zamani wa Arsenal na mkali ambaye aliitesa sana Liverpool wakati wake.
- Luis Suarez: Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool anayeichezea Barcelona
- Fernando Torres: Mkali wa mabao wa zamani wa Liverpool anayeichezea Atletico Madrid hivi sasa.
JAMIE CARAGHER
- Pepe Reina: Kipa aa Zamani wa Liverpool anayeichezea Bayern Munich hivi sasa.
- Peter Gulacsi: kipa wa zamani wa Liverpool anayeidakia Red Bull Salzburg
- Alvaro Arbeloa: Beki wa zamani wa Liverpool anayeichezea Real Madrid.
- Jamie Carragher: The man himself (Mhusika mkuu)
- Gael Clichy: Beki wa Manchester City
- Martin Kelly: Beki wa Crystal Palace na mchezaji wa zamani wa Liverpool
- Luis Garcia: kiungo wa Atletico De Kolkata ambaye alikipiga pia Liverpool
- Craig Noone: Kiungo wa Cardiff City
- Stewart Downing: kiungo wa West Ham midfielder na mchezaji wa zamani wa Liverpool
- Jonjo Shelvey: kiungo wa Swansea City ambaye ameitumikia pia Liverpool
- Harry Kewell: Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool
- Craig Bellamy: Mshambuliaji wa zamani Liverpool
- Didier Drogba: mshambuliaji wa Chelsea


No comments