KWA HILI LA OSCAR, JOSE MOURINHO UNANIDANGANYA
.... Na Zahir Bilal
Katika kitongoji cha Americana nchini Brazil tarehe 9/9/1991 alizaliwa "Oscar Emboaba Dos Santos Jr" maarufu kama Oscar
Ni mchezaji wa kwanza aliyewahi kufunga hat trick (Magoli matatu) katika fainali ya kombe la dunia chini ya miaka 20 ilikua dhidi ya Ureno mwaka 2011.
Alianzia safari yake ya soka katika timu za União Barbarense ,Sao Paulo na Internacional za nchini kwao Brazil kabla ya kuonwa na kuvutwa na pesa za mrusi Roman Abramovich pale London katika timu ya Chelsea.
Soka lake zuri pasi za uhakika na magoli ya kuvutia kiasi cha paundi milion 19.35 zilizotumika kumng'oa Internacional zilikua ni sawa na wizi wa mchana kweupe na aliithibishia dunia hilo chini ya wakufunzi Andre Vilas Boas,Roberto Di Matteo na Rafael Benitez, na dunia iliamini Brazil ilikua imempata Ricardo Izecson Dos Santos Leite 'Kaka' mpya,na pale darajani wakatengeneza utatu wa hatari uliofahamika kama MAZACAR yaani Mata, Hazard na Oscar utatu huu ulikuja kuvunjwa baadae na mbabe mmoja kutoka Ureno Jose Mourinho.
Huwa najiuliza Oscar huyu ndio yule yule aliyekuwa anafunga magoli ya mita 20,25 hadi 30? jibu ni hapana bado nayakumbuka zaidi yale magoli yake mawili maridhawa dhidi ya Gigi Buffon.
Uhodari wake wa kucheza nyuma ya mshambuliaji unapunguzwa zaidi na mbinu za José anayetaka mchezaji acheze mara mbili zaidi ya vile anavyocheza ,siku hizi umahiri wake hauamui mechi za Chelsea tena kwa sababu anafanya kazi nyingi na kukimbia kilomita nyingi zaidi kuliko kazi aliyoletwa kufanya duniani ya kupika mabao pamoja na kufunga matokeo yake anacheza katika kivuli cha Fabregas na Hazard na Mou kusahau miguu yake murua ya almasi ambayo ikitumika inavyotakiwa huleta madhara zaidi ya zile mbio za Eden Hazard.


No comments