●● INSIDE UNITED●● HAWA NDIYO WACHEZAJI WA UNITED WANAOZITUMIKIA TIMU ZAO ZA TAIFA.


Kama ilivyo kawaida wiki hii ni wiki ambayo inatawaliwa na mechi za kimataifa katika kalenda ya FIFA Ligi mbalimbali duniani zimesimama kupisha mechi hizi huku wachezaji wakipata muda wa kuzichezea timu zao za Taifa

Leo katika INSIDE UNITED tunaangalia wachezaji wa Man United ambao wataziwakilisha timu za mataifa yao katika mechi za kirafiki pamoja na kufuzu kwa Kombe la mataifa ya Ulaya.

United imetoa wachezaji wanne katika kikosi cha Timu ya Taifa ya England na wote wanaweza kucheza kutokana na viwango vyao kuwa bora hivi sasa Chriss Smalling,Phil Jones,Michael Carick na nahodha Wayne Rooney wote wamo katika kikosi cha England ambapo kesho Ijumaa wataialika Lithuania katika mechi ya Kundi E kuwania nafasi ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Ulaya mechi itapigwa katika dimba la Wembley.

England baada ya mechi hiyo itasafiri mpaka Italia kuwavaa Italia katika mechi ya kirafiki siku ya Jumanne.

Marouane Fellaini ambaye amekua muhimuli muhimu katika matokeo ya Man United siku za hivi karibuni atakua akiitumikia timu yake ya Taifa ya Ubelgiji katika mechi za kufuzu dhidi ya Cyprus na Israel.

Johnny Evans na Paddy McNair wao jana walikua wakiiwakilisha Ireland ya kaskazini walipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Majirani zao Scotland na badae wataiwakilishi nchi yao kupambana na Finland katika kutafuta nafasi ya kufuzu.

Radamel Falcao ambaye uwepo wake Man United umezusha maswali mengi wengi wakijiuliza juu ya mkali huyu wa kupachika mabao yeye atakua katika kikosi cha Colombia watakaoivaa  Bahrain leo kabla ya kucheza na Kuwait Jumapili katika mechi za Kirafiki za Kimataifa.

Daley Blind ni mchezaji mwingine katika orodha ya wakali wa Man United atakayekua na timu yake ya Taifa ya Uholanzi watakaoivaa Uturuki katika kundi A kutafuta nafasi ya kufuzu Ulaya badae Jumanne wataialika Spain katika mechi ya kirafiki.

David De Gea akiwa katika kiwango bora kabisa anatarajiwa kuwepo golini wakati Spain watakapopambana na Ukraine katika kutafuta nafasi ya kufuzu Ulaya akiwa ndo mchezaji pekee katika kikosi cha spain.

Angel Di Maria na Marcos Rojo nao watakua uwanjani wakiwa na kikosi cha Argentina dhidi ya El Salvador na badae kuwakabili wakina Valencia ambaye atakua na timu yake ya Taifa ya Ecuador katika mechi za kirafiki.

.... KWA LEO NI HAYO TU KATIKA INSIDE UNITED TUKUTANE TENA KESHO KUANGALIA NINI KINACHOENDELEA NDANI YA KLABU YA MANCHESTER UNITED.


Enjoy

a

No comments

Powered by Blogger.