KOCHA WA ITALIA ATISHIWA KUUAWA
Kocha wa Timu ya Taifa ya Italy ambaye zamani aliinoa Juventus Antonio
Conte ametishiwa kuuawa kufuatia Mchezaji wa Juventus Claudio Marchisio kuumia vibaya Goti wakati akiwa Mazoezini na Italy.
Mashabiki wenye hasira walitoa Vitisho hivyo katika Mitandao ya jamii na wanasadikiwa ni Mashabiki wenye hasira wa Juventus ambao ndio Mabingwa Watetezi na Vinara wa Serie A .
Mtendaji mkuu wa kampuni ya Magari ya FIATI Ambao ni wamiliki wa klabu ya Juventus John Elkann amemlaumu vikali Conte kwa mazoezi yake wakati Conte yeye anamshangaa John kwamba wakati yuko Juventus hakuwahi kulalamikia mazoezi lakini hivi sasa yuko timu ya Taifa imekua ni shida.
Marchisio aliumia Goti wakati wa mazoezi Ijumaa na Conte anasema mchezaji huyo aliumia akiwa peke yake akikimbia bila hata ya mpira katika mazoezi ya matayarisho yao kwa Mechi ya Jumamosi dhidi ya Bulgaria Kundi H la kufuzu EURO 2016 na sasa Mchezaji huyo atakuwa nje ya Uwanja hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Hivi sasa huko Italy zipo habari kuwa Conte anatafakari hatima yake katika kuifundisha Italia baada vitisho hivi vya maisha yake japo yeye mwenyewe au Shirikisho la Soka la Italy halijazungumzia hilo.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments