TETESI ZA USAJILI WA WACHEZAJI BARANI ULAYA
Manchester United wameanzisha dili tata la kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale mwenye miaka 25.
Inasemekana kiasi cha paundi milion 100 zimetengwa kukamilisha dili hilo huku kukiwa na taarifa za kumuhusisha pia David De Gea kutimkia Madrid katika dili hilo
. (Sunday People)
Taarifa nyingine inasema kuwa Real Madrid wako tayari kuvunja rekodi ya dunia kumsajili David De Gea bila kumhusisha Gareth Bale.
(Daily Star Sunday)
Wakati huo huo Manchester United wanataka kuanzisha majadiliano ya dau la uhamisho paundi milion 43 kuilipa Monaco kama wataamua kumbakiza Radamel Falcao ambaye anakipa kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu huu.
(Daily Telegraph)
Arsenal, Liverpool na Manchester City wote wamemtolea macho Falcao kutaka kumsajili kama United watamwachia baada ya mkopo kuisha.
(Sunday Times )
Tottenham Hotspur wameanzisha tena mpango wa kumsajili winga wa Dnipro ya Ukraine mwenye miaka 25 ambaye mkataba wake unaisha mwezi June Yevhen Konoplyanka.
(Mail on Sunday)
Liverpool watamruhusu mshambuliaji Rickie Lambert mwenye miaka 32, kuondoka klabuni hapo kama wataweza kumrudisha Divock Origi aliye kwa mkopo katika klabu ya Lile ya ufaransa.
(Sun )
Borussia Dortmund imeanza kumnyemela mshambuliaji wa Everton Kevin Mirallas mwenye miaka 27, ambaye mkataba wake umebaki miezi 18 kumalizika
.(Sunday People)
Manchester United na Chelsea wana matumaini ya kumsajili Luka Modric kutoka Real Madrid baada ya taarifa kuzagaa kuwa mke wa Modric hana furaha kukaa katika jiji la Madrid.
(Sunday Express)
Bosi mpya wa Crystal Palace Alan Pardew anataka kumsajili mshambuliaji Papiss Cisse kutoka Newcastle
(Sunday Mirror)
Kocha wa Real Sociedad David Moyes anasubiri jibu kutoka kwa bosi wa Arsenal Arsene Wenger kutaka kumsajili mshambuliaji Joel Campbell kwa mkopo
(Sunday People)

No comments