TETESI ZA USAJILI JIONI YA LEO BARANI ULAYA
Kocha wa West Brom Tony Pulis amepeleka ofa ya paundi milionu 4 kutaka kumsajili Winga wa Wigan Callum McManaman mwenye miaka 23 lakini Wigan wanaema thamani ya mchezaji huyo ni paundi milioni 6 sio 4.
(Daily Telegraph)
Swansea wameweka mezani paundi milioni 4 kumwania beki wa Norwich City Martin Olsson. (Daily Express)
Manchester United wana matumaini ya kumsajili mshambuliji wa Real Madrid Gareth Bale, kwa paundi milion 40 pamoja na kumpeleka kipa David De Gea, ambaye anaaminika thamani yake kufikia paundi milioni 40 hivyo kufanya dili hilo kuwagharimu Man United paundi milioni 80
. (Manchester Evening News)
Liverpool wanaonekana wanakaribia kumsajili kiungo wa Ipswich Teddy Bishop, mwenye miaka 18, ambaye amejihakikishia namba katika kikosi cha Ipswich kinachoshiriki ligi daraja la kwanza Championship
(Daily Mirror)
Kiungo wa Villarreal Gabriel Paulista mwenye miaka 24 amesema kuwa Wakala wake anaendelea na maongezi na Arsenal kuhusu kusajiliwa na wakali hao wa London katika usajili wa Januari.
. (Guardian)
Mkali wa Mabao wa Burnley Danny Ings mwenye miaka, 22, ambaye mkataba wake unamalizika mwezi June amesema mazungumzo kuhusu mkataba mpya na timu hiyo inayotumia uwanja wa Turf Moor yanazidi kufifia na hii inatoa mwanya kwa wale wanaomhitaji
(Sky Sports)

No comments