TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA SIKU YA JANA ALHAMISI


DAVID DE GEA

Baada ya mkakati wa kumng'oa katika kikosi cha Man United kipa David De Gea kushindikana Real Madrid wameamua kumsubiri David De Gea mpaka mkataba wake utakapoisha ili wamsajili bure.
(Daily Telegraph)

EMMANUEL ADEBAYOR:

Paris St-Germain wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa  Tottenham Emmanuel Adebayor, mwenye miaka 30 kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu.
(Daily Telegraph)

RUDY GESTEDE:

Swansea City wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Blackburn striker Rudy Gestede, 26, lakini mpaka sasa wameshindwa kufikia dau la paundi milioni 6 ambalo Blackburn wanalitaka.
(Daily Mail)

RUBEN NEVES:

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anajiandaa na dau la paundi milioni 29 kuwapiku PSG,Real Madrid na Juventus kumsajili kinda wa miaka 17 Ruben Neves ambaye anajulikana kama  Sergio Busquets mpya akiichezea FC Porto kwa sasa
 (Daily Express)

BAFETIMBI GOMIS:

West Ham wameweka dau la paundi milioni 8 kwa mshambuliaji wa Swansea mwenye miaka  29 Bafetimbi Gomis. Gomis amefunga magoli manne katika mechi 24 msimu huu akiichezea Swansea.
(Sun)

JACKSON MARTINEZ:

Wakala wa mshambuliaji wa Porto Jackson Martinez, 28, amekataa dili la mchezaji huyo kujiunga na  Tottenham, Liverpool au Everton ili akacheze katika ligi ya Italia Serie A,
(Daily Express)

NICK POWELL:

Kiungo wa Manchester United Nick Powell, 20, anaweza kupelekwa Hull City ili kukiendeleza kipaji chake chini ya kocha Steve Bruce.
 (Daily Mirror)

JORDON MUCH & PAPE SOUARE

Crystal Palace wako mbioni kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Queens Park Rangers Jordon Mutch, 23, kwa kiasi cha £4.75m na beki wa Senegal anayekipiga Lille ya Ufaransa  Pape Souare, 24, kwa kiasi cha £3.4m
.(Guardian)

2 comments:

  1. Ukiskia Nyota Ndo hii kwa Emmanuel adebayor aisee jamaa ana nyota ya chips team anazopita zote za uhakika

    ReplyDelete
  2. Yah jamaa ana kismati ila awashukuru sana Man City kwani mshahara wake kwani hakuna anayeweza kuushusha ukitaka kumsajili

    ReplyDelete

Powered by Blogger.