SIMBA NA AZAM HAKUNA MBABE WAKATI MTIBWA WACHAPWA MABATINI
Ligi kuu ya soka Tanzania Bara iliendelea leo kwa viwanja kadhaa kuwa katika wakati mgumu kwa michezo mbali mbali kupigwa katika viwanja hivyo.
Ligi hiyo ambayo inadhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ilishuhudia mabingwa watetezi Azam FC wakibanwa mbavu na Simba SC kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika pambano lililopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
SImba walitangulia kupata bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji wake Emmanuel Okwi akipiga mpira wa mbali uliomshinda kipa Mwadini na kuiandikia Simba bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Azam walionekana kuimarika zaidi na mabadiliko ya kuwaingiza John Bocco na Mcha Hamisi yalifanikisha kupatikana goli la kusawazisha kupitia kwa Kipre Tchetche na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Emmanuel Okwi alitolewa katika mchezo huo akiwa katika machela baada ya kuzimia uwanjani.
wakati huo huo Mtibwa Sugar iliambulia kichapo cha bao 2-1 toka kwa Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliopigwa katika uwanja wa mabatini pale Kibaha..
MATOKEO YOTE YA MECHI ZA LEO
- Azam FC 1-1 Simba SC
- Ruvu Shooting 2-1 Mtibwa
- Kagera Sugar 1-2 Ndanda FC
- Stand United 0-1 Coastal Union
- Mbeya City 2-2 Prisonsu
- JKT Ruvu 1-1 Mgambo

No comments