AFCON 2015 ~ WENYEJI EQUATORIAL GUINEA NA CONGO WATINGA ROBO FAINALI



Hatu ya mwisho ya mechi za makundi ya michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2015) Imeanza jana kwa wenyeji Quatorial Guinea kuwatupa nje majirani zao Gabon katika mechi za kundi A la michuano hiyo.


Equatorial Guinea ikichagizwa na mashabiki wao walioujaza uwanja jijini Malabo waliitandika Gabon bao 2-0 magoli ya wenyeji yakiwekwa kimiani na Javier Balboa kwa njia ya penati huku Salvador Edu akifunga bao la ushindi zikiwa zimebaki dakika nne mpira kumalizika.

Katika mechi nyingine ya Kundi A Congo Brazaville ambayo Wapenda Soka wengi hatukuipa nafasi iliibamiza Burkina faso bao 2-1 magoli ya washindi yakiwekwa kimiani na Thievy Bifouma dakika ya 51 na Fabrice Ondama N'Guessi huku Burkina Faso wakipata bao la kufutia machozi kupitia Aristide Bance dakika moja kabla ya Congo kupata bao la ushindi.

RATIBA YA MECHI ZA LEO 26/01/2015

KUNDI B
9:00 PM - Cape Verde Islands vs Zambia
9:00 PM - Congo DR vs Tunisia.

NOTE: MECHI ZOTE ZINACHEZWA MUDA MMOJA KUEPUKA KUPANGA MATOKEO.

No comments

Powered by Blogger.