SIMBA HOI KWA MBEYA CITY: YACHAKAZWA VIBAYA TAIFA.



  • Yachapwa 2-1 Uwanja wa Taifa 
  • Chollo akosa penati ya dakika za mwisho

Ligi kuu ya Soka Tanzania bara maarufu kama Vodacom Premier League imeendelea tena jioni hii kwa mechi kali kati ya Simba SC toka Kariakoo Jijini Dar es Salaam walipowakaribisha Wananchi wa Mbeya klabu ya Mbeya City katika dimba la Taifa Jijini.


Ikiwa katika dimba lake hilo Simba ilikubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Mbeya City mchezo uliotawaliwa na ufundi mwingi,kasi ya ajabu na ubabe wa hapa na pale.

Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi walianza kupata bao lililofungwa na mshambuliaji wake Ibrahim Hajib kipindi cha kwanza na kupelekea pambano hilo kwenda Mapumziko Simba wakiongoza.

Kipindi cha pili Mbeya City walikuja na nguvu mpya na kushambulia lango la Simba kama nyuki huku wakicheza pasi fupi fupi zilizoonekana kuwachosha kabisa Simba na kushindwa kuwakabili Mbeya City ambao waliweza kupata mabao mawili kipindi cha Pili moja likifungwa kwa ustadi mkubwa na Hamad Kibopile kabla ya Manyika Peter hajamfanyia madhambi mchezaji wa Mbeya City na mwamuzi kuamuru kupigwa penati dakika za mwisho kabisa penati iliyofungwa kiufundi na Yusuph Abdalah.

Simba nao walipata penati dakika zikiwa zimeisha kabisa baada ya Mkude Jonas kuangushwa ndani ya eneo la hatari na kwa bahati mbaya Masoud Chollo aligongesha mwamba na kukosa penati hiyo
Hivyo mpaka mwisho wa mchezo Simba 1-2 Mbeya City.

~ Edo DC

No comments

Powered by Blogger.