LUIS FIGO AJITOSA KUWANIA URAIS WA FIFA
Mkali wa Soka toka Ureno Luis Figo amekua mtu wa mwisho Kutangaza nia ya kugombea Uraisi wa FIFA akitaka kumpa Changamoto Rais wa sasa Sepp Blatter.
Katika kile kinachoonekana kuwa waliokua wachezaji wa soka kuamka Figo anakua mchezaji wa pili wa zamani kutangaza kuwania nafasi hiyo akiungana na David Ginola ambaye wiki iliyopita alijitokeza na kutangaza kuwania nafasi hiyo kubwa katika soka wakiwania kumwondoa madarakani raisi wa sasa Sepp Blatter.
Mtoto wa Mfalme wa Jordan Prince Ali, Mholanzi Michael Van Praag na Jerome Champagne nao wako katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais wa FIFA.
Sepp Blatter amekua rais wa FIFA tangu mwaka 1998 na ameshatangaza kugombea kwa mara ya 5.
Figo akiwa mmoja wa watakaogombea Urais ametanabaisha kuwa "Mpira umenipa mambo mengi maishani nami nataka kulipa fadhila"
Figo amecheza mechi 127 akiwa na timu ya taifa ya Ureno na alishinda pia Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2002 akiwa na Real Madrid.


No comments