REAL MADRID NDIYO TIMU TAJIRI ZAIDI DUNIANI, MAN UNITED YAFATIA


Kampuni ya kimataifa inayojihusisha na ukaguzi wa makumpuni Delloitte imetoa orodha ya timu za soka zinazoongoza kwa utajiri duniani huku mabingwa wa Ulaya Real Madrid, wakishika nafasi ya kwanza katika orodha ya timu tajiri kuliko zote duniani kwa mwaka wa 10 mfululizo.


Manchester United imesogea hadi nafasi ya pili kutoka nafasi ya nne, katika tathmini hiyo ambayo hufanywa kwa kuangalia mapato ya klabu husika kwa msimu mzima na hii iliyotoka sasa ni tathimini ya mapato ya msimu wa 2013-14.

Bayern Munich ambao ni mabingwa wa Ujerumani wanakamata nafasi ya 3, Barcelona nafasi ya 4 na Paris Saint-Germain imeibuka namba 5.

Klabu za England za Manchester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool zimo katika kumi bora ya klabu tajiri, zote zikionesha ongezeko zuli la mapato.

Na hii ndiyo Orodha kamili ya kumi bora pamoja na mapato yao kwa msimu wa mwaka 2013-14 ni kama ifuatavyo kwa sarafu ya Euro:
(Kwenye mabano ni mapato ya msimu wa 2012-13)

•1. Real Madrid: 549.5m (518.9m)

• 2. Man Utd: 518m (423.8m)

• 3. Bayern Munich: 487.5m (431.2m)

• 4. Barcelona: 484.6m (482.6m)

• 5. Paris Saint Germain; 474.2m (398.8m)

• 6. Manchester City: 414.4m (316.2m)

• 7. Chelsea: 387.9m (303.4m)

• 8. Arsenal: 359.3m (284.3)

• 9. Liverpool: 305.9m (240.6m)

• 10. Juventus: 279.4m (272.4m)

No comments

Powered by Blogger.