CAMBRIDGE UNITED VS MAN UNITED : PAMBANO LA DAUDI NA GOLIATH


Uwanja : Abbey Stadium
Uwezo : mashabiki 8,127
Tarehe: 23 Januari 2015 (Ijumaa)
Muda : 10:45 PM



Raundi ya 4 ya kombe la FA inaendelea leo usiku kwa mechi moja tu kupigwa katika dimba la Abbey nyumbani kwa Cambridge katika ya Mancheter United na timu ya darasa la pili ya Cambrige United katika mchezo utakaoanza majira ya saa 5 kasorobo usiku.
Pambano kati ya timu kubwa sana duniani na England na timu ndogo zaidi wengi wakilifananisha na pambano la Daudi na Goliath katika Biblia

VIKOSI

Kwa Upande wa Man United Mshambuliaji wa wake Robin van Persie na beki wa timu hiyo Luke Shaw na Rafael wanaweza kuwemo katika kikosi cha leo usiku hawa wote walikua majeruhi
Lakini Ashley Young, Chriss Smalling na John Evans wataikosa mechi hiyo kutokana na kuwa majeruhi.

Kwa Upande wa Cambridge ambayo wachezaji wake karibia wote hawajanunuliwa kutoka timu yoyote itakua faraja kwao kucheza na Man United ambayo ni timu yenye mafanikio zaidi katika soka la England.
Inaweza kumtumia beki Dominic Ball ambaye wamemsajili kutoka Totenham kwa Mkopo

Wakati Man united ikikamata nafasi ya 4 katika msimamo wa ligi kuu,Cambridge wao wako nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi daraja la pili na pengine hili ndilo kombe pekee ambalo Man United wakikomaa wana weza kulipata baada ya kukosa Ligi ya Mabingwa huku mbio za kusaka ubingwa katika Ligi zikiwa ndefu sana kwao.

++++++++++++++++++++++++

HISTORIA

Cambridge United imekutana na Manchester United mara moja tu ilikua ni mwaka 1991 katika kombe la Ligi.
Mechi ya kwanza Man united ikishinda bao 3-0 Old Trafford kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dimba la Abbey Cambridge.

Cambridge United imefika robo fainali ya michuano hiyo mara mbili katika historia yake. Mwaka 1990/1991 na mwaka 1991/1992

Kwa upande wa Man United imeshinda kombe la FA mara 11 japokua ushindi wake wa mwisho wa kombe hilo ilikua zaidi ya miaka 10 iliyopita yani mwaka 2004.

Manchester United wamepoteza mchezo mmoja tu katika michezo 13 iliyopita katika mashindano yote. Huku Wayne Rooney akifunga magoli 6 katika mechi 6 zilizopita za kombe la FA akiwa na United.


No comments

Powered by Blogger.