POGBA ATAONDOKA JUVENTUS - WAKALA

Paul Pogba

Wakala wa kiungo wa Kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba mchezaji anayekipiga katika klabu ya Juventus ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini Italia Serie A amefunguka na kusema kiungo huyo ataondoka Juventus ndani ya miaka miwili Ijayo.


 Pogba ambaye ana miaka 21 alijiunga na Juventus akitokea  Manchester United mwaka 2012 na ameshafunga bao 8 katika michezo 26 aliyoichezea Juventus msimu huu.

Wakala wa kiungo huyo Mino Raiola ameviambia vyombo vya habari leo kama ikitokea Pogba ameondoka Juventus basi itakua katika uhamisho wa juu kabisa na anaamini Pogba ataondioka msimu ujao sio msimu huu.
Mino Raiola akiongea na waandishi wa habari
"Katika wakali wa soka wanaotikisa dunia hivi sasa Paul pekee ndiye pekee anaweza kusajiliwa na timu yoyote baada ya msimu ujao.
Yani kama utashindwa kumsajili Cristiano Ronaldo,Lionel Messi na Zlatan Ibrahimovic mtu pekee unayeweza kumsajili ambaye yuko katika kiwango cha juu na anapatikana ni Paul Pogba" Alisema Wakala huyo.

Ikumbukwe kuwa Paul Pogba aliihama Man United kwa dau la paundi 800,000 miaka miwili na nusu iliyopita lakini anaweza kusajiliwa kwa dau la uhamisho Euro 100m hivi sasa  kuvunja rekodi ya Gareth Bale ya paundi milioni 85.3

+++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.