MAN CITY WAMTAKA MESSI SASA, ARSENAL WAKOMAA NA MATTS HUMMELS NA GUNDOGAN,SCHURRLE NA SALAH KUPIGWA BEI CHELSEA


Kocha wa Manchester City manager Manuel Pellegrini amefunguka na kusema anamtaka Lionel Messi na wako tayari kutoa paundi milion 480 kumhamisha toka Barcelona
  ( The Sun )




Arsenal wako tayari kuanza mazungumzo na  Borussia Dortmund. Wakitenga paundi milion 65 kuwasajili kiungo Ilkay Gundogan na mlinzi wa kati Mats Hummels
....  (Star)

Klabu ya Palermo imesema imekataa maombi ya   Manchester United kutaka kumsajili mshambuliaji chipukizi wa klabu hiyo mwenye miaka 21 raia wa Argentina  Paulo Dybala wakidhani kuwa ana thamani ya paundi milion 30 ambayo Man United wanaiona ni kubwa mno.
... (Guardian)

Paris St-Germain, Porto na Juventus wote wamevutiwa na dili la kumsajili kwa mkopo winga Adnan Januzaj mwenye miaka 19 kutoka Manchester United..
 (The Sun )


Crystal Palace wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa  Swansea City Bafetimbi Gomis mwenye miaka 29 ambaye thamani yake ni paundi  milion 8
(Times)

Kocha mpya wa West Brom Tony Pulis anajiandaa kupeleka dili la kumsajili kiungo wa  Manchester United Darren Fletcher mwenye miaka 31 ambaye inasemekana ameshaonyeshwa mlango wa kutokea Old Trafford.
 (Express and Star)

Swansea wanajiandaa kutumia pesa walizopata kwa kumuuza  Wilfried Bony kwenda Manchester City kumsajili kiungo wa Stuttgart Alexandru Maxim mwenye miaka 24 ambaye thamani yake ni paundi milion 5..
(Telegraph)


Manchester United wamefungua mazungumzo na PSG ya Ufaransa kutaka kumsajili beki raia wa Brazil mwenye miaka 20 Marquinhos
.(Le10sport)

Mkataba mpya wa mshambuliaji  Charlie Austin mwenye miaka 25, na klabu yake ya QPR unasuasua na hivyo kuweka vilabu vingine vinavyomwania katika matumaini ya kumsajili.
(Mail)


Liverpool wanamwania kipa wa Australia Mathew Ryan mwenye miaka 22, ambaye anakipiga katika klabu ya Bruges ya Ubelgiji ili kuja kugombania namba na makipa waliopo klabu hapo hasa Simon Mignolet.
 (Express)


Tottenham wameungana na Arsenal kumwania mlinzi wa West Ham ambaye ni raia wa New Zealand mwenye miaka 26 Winston Reid. (Telegraph)


Kocha wa Chelsea Jose Mourinho yuko tayari kupunguza idadi ya mawinga klabuni hapo kwa kuwauza  Andre Schurrle mwenye miaka 24, na Mohamed Salah mwenye miaka 22 na kutumia pesa zitakazopatikana kumsajili mlinzi wa Real Madrid Raphael Varane mwenye miaka 21.
 (Star)


Mshambuliaji wa Everton Kevin Mirallas mwenye miaka 27, amesema ataamua wapi atacheza soka baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi
 (Liverpool Echo)

No comments

Powered by Blogger.