MAAJABU KOMBE LA FA - CHELSEA,MAN CITY,SOUTHAMPTON NA SPURS ZATUPWA NJE..
![]() |
| Patrick Blomfed akishangilia goli alilowafunga Man City |
Mechi hizo za Raundi ya nne zimemalizika muda mfupi uliopita na kushuhudiwa Vinara wa Ligi Kuu England Chelsea wakitupwa nje kwa kufungwa bao 4-2 nyumbani kwao Stamford Bridge na klabu ya daraja la Championship Bradford City.
![]() |
| Wachezaji wa Chelsea wakitoka uwanjani vichwa chini |
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Nchini England Manchester City wao walikubali kichapo cha bao 2-0 nyumbani Etihadi toka kwa Middlesbrough timu nyingine inayoshiriki Championship.
Southampton ambao msimu huu wameonekana wako vizuri na kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi walikubali kichapo cha bao 3-2 toka kwa Crystal Palace ambayo imeongezwa nguvu kufatia kumpata kocha mpya Allan Pardew pambano hilo lilipigwa nyumbani kwa Southamptob St. Marys stadium.
![]() |
| Chamakh,zaha,campbel na Sanogo wakishangilia |
Klabu zingine za Ligi kuu ambavyo vimepata vichapo leo ni pamoja na Swansea City waliokubali kichapo cha bao 3-1 toka kwa Blackburn Rovers ambayo nayo inashiriki Ligi ya Championship.
MATOKEO YOTE YA KOMBE LA FA LEO
- Blackburn Rovers 3-1 Swansea
- Birmigham City 1-2 West Brom
- Cardiff City 1-2 Reading
- Chelsea 2-4 Bradford City
- Derby County 2-0 Chesterfield
- Manchester City 0-2 Middlesbrough
- Preston 1-1 Sheffield United
- Southampton 2-3 Crystal Palace
- Sunderland 0-0 Fulham
- Tottenham Hotspurs 1-2 Leicester City



No comments