LIGI KUU TANZANIA BARA - YANGA YAWAVAA MAAFANDE MOROGORO



Hatua ya 12 ya ligi kuu nchini Tanzania Maarufu kama Vodacom Premier League itaendelea leo kwa mechi moja tu kati ya mabingwa wa Kihistoria Yanga watakaokua ugenini kuikabili timu ngumu ya Polisi Morogoro.


Yanga itaingia katika mechi ya leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya sare dhidi ya wanajeshi wa Ruvu Shooting pambano ambalo lilitawaliwa na ubabe mwingi na kupelekea mwamuzi wa pambano hilo kufungiwa miaka mitatu kwa kushindwa kumudu mchezo.

Mechi zingine zitakua kesho Ambapomabingwa watetezi Azam watapepetana na Simba ambao ni mabingwa wa kombe la Muungano.
Kagera Sugar itaikaribisha Ndanda FC
Stand United wataialika Coastal Union
Mbeya City watacheza na Prisons
Ruvu Shooting wataialika Mtibwa Sugar
JKT Ruvu watawaalika Mgambo

No comments

Powered by Blogger.